• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Hizi Pesa Ni Zenu Wananchi-Claudia U. Kitta

Imewekwa Kwenye: December 17th, 2020

Haya yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Claudia U.kitta alipokuwa akiongea na vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, katika hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi ya mikopo yenye thamani ya shilingi 140,000,000/= .

Hafla hii imeandaliwa na Idara ya maendeleo ya jamii iliyofanyika katika ukumbi mkubwa wa halmashauri ya wilaya ya Kyela tarehe 16/12/2020.

Akizungumza kabla ya kukabidhi Hundi hiyo Mhe.Mkuu wa wilaya amesema, Hii ndio serikali inayongozwa na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Na serikali hii inatimiza maagizo yote yaliyopo katika ilani ya chama. Hata utoaji wa mikopo hii kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wanye ulemavu ni sehemu mojawapo ya utekelezaji wa ilani ya chama chetu.

Aidha Mkuu wa wilaya amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel H.Magehema kwa uwezo wake mkubwa wa kukusanya mapato ya serikali hadi kasababisha mikopo hii kutolewa kwa wakati.

Pia Mhe.Claudia U. Kitta amewataka wanavikundi kuwa na umoja ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea. Sababu pesa hizi ni kodi kutoka kwa wananchi, hivyo pesa hizi ni zao na wanapaswa kurejesha kwa muda ili kuwasaidia wananchi wengine.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela amesema, Kyela ni wilaya ambayo watu wake wakiamua kubadilika wataleta maendeleo makubwa katika wilaya. Kwani Kyela ni wilaya yenye fulsa nyingi ukilinganisha na maeneo mengine.

Hivyo aliwataka wanavikundi kutumia mikopo hii katika fulsa zilizopo Kyela, mfano upatikanaji wa michikichi, kokoa, mpunga na vitu vingine vingi. Pia aliwaasa wanavikundi kujiunga na mfuko wa iCHF ili wanapopata matatizo ya afya mfuko huo wa bima ya afya uwasaidie na si kutumia hela ya mkopo kwa matibabu.

Akizungumza kwa niaba ya wanavikundi Bi.Rehema Kalisa alitoa pongezi kwa viongozi wa wilaya kwa kuwawezesha wananchi kupata mikopo yao kwa wakati, aliwawaahidi viongozi hao kwenda kutumia mikopo hiyo kwa maendeleo ya jamii nzima.

Halmashauri ya wilaya ya Kyela imetoa mikopo kwa vikundi 27 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu, mikopo wenye thamani ya shilingi 140,000000/=.

Baadhi ya wanavikundi wakionesha bidhaa zao kwa viongozi bidhaa ambazo zimeyokana na mikopo kutoka serikalini.

Matangazo

  • Kikao Cha Balaza La Waheshimiwa Madiwani Kesho Tarehe 02/03/2021 March 01, 2021
  • Matokeo Kidato Cha Nne 2020 January 21, 2021
  • Orodha Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati 2020 June 17, 2020
  • Orodha Ya Majina Ya Walioteuliwa Kuwa Wasimamizi Na Makarani Waongozaji Katika Uchaguzi Mkuu October 28th 2020 October 19, 2020
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Tuilinde Miradi Inayotekelezwa Na Serikali-Albert Chalamila

    February 25, 2021
  • Sherehe Za Maazimisho Ya Kuzaliwa Kwa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Wa Mbeya Zafanyika Wilayani Kyela

    February 05, 2021
  • Serikali Ya Gharamia Zaidi Ya Shilingi Bilioni tatu (3,000,000,000) Kujenga Mradi Wa Maji Kyela

    January 02, 2021
  • Mheshimiwa Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Kyela Afanya Ziara Katika Ujenzi Wa Vyumba Vya Madarasa

    December 29, 2020
  • Angalia Zote

Video

RAIS MAGUFULI AKIWA SONGEA
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0756944794

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa