Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Hunter Mwakifuna, amewataka wananchi wa Kyela kuachana na mila potofu zinazowapelekea kujiingiza katika maswala ya ukatili wa kijinsia.
Amezungumza haya siku ya tarehe 06/03/2020, katika kata ya Ipinda wilayani Kyela alipokuwa akifungua mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyokuwa yakitolewa na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kyela kupitia ofisi ya Maendeleo ya Jamii.
Akizungumza na makundi ya wazee maarufu, viongozi wa dini, watendaji kata amesema, Wananchi wengi katika wilaya ya Kyela wamejiingiza katika ushirikina katika kutafuta mali, ambapo wengi wamekuwa wakiwabaka vikongwe pamoja na kuwalawiti watoto wadogo. Jambo hili linapelekea uchochezi wa ukatili wa kijinsia katika wilaya yetu.
Aidha alikemea baadhi ya tabia za wazazi ambao ndugu zao au watoto wao wamefanyia ukatili, kuachatabia ya kusema kuwa, wanandugu wamemalizana kwani tabia hii si nzuri, kwani anaekuwa kafanyiwa vitendo hivyo ni mtoto na ndie alieathilika hivyo wazazi hawapaswi kufuta kesi kama hizo na inawapasa kuheshimu sheria na haki zitendeke.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo wa wilaya ya Kyela Ndugu Victor Kabuje alisema, wamejipanga kukabiliana na wazazi wote ambao wamekuwa wakifuta kesi kwa sababu ya kusema wamemalizana, na hata hivyo wameanza kwa kwa kutoa elimu kwanza, na elimu hii wanategemea kuifikishia jamii yote ya Kyela kwa kupitia makundi mbalimbali.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa