Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania jana tarehe 20/03/2019 imekabidhi msaada wa tani 200 za mahidi, vyandarua, magodoro pamoja na dawa za binadamu tani 15, kwa Nchi ya Malawi iliyokumbwa na kimbunga kiitwacho Idai.
Msaada huo umekabidhiwa wilayani Kalonga Nchini Malawi, ambapo Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Willium Paulo uliukabudhi Mzigo huo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.
Aidha Mhe. Willium Paulo amesema, msaada huu umetolewa na nchi ya Tanzania kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo baina na nchi ya Tanzania na Malawi.
Akipokea Msaada huo, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya wa Malawi ndugu. Raphael Mkisi amesema, anaishukuru sana nchi ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa ulio onyeshwa na nchi ya Tanzania kwa nchi ya Malawi, ameomba ushirikiano huu na uendelee kudumu zaidi na zaidi.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Claudia U. Kitta alisema, utoaji wa msaada huu umetolewa kwa sababu nchi ya Tanzania imeguswa sana juu ya maafa haya ambayo nchi rafiki, jirani imeyapata.
Takribani wilaya 13 kutoka mikoa 7 ya Malawi zimekumbwa na kimbunga hiki cha Idai, na watu zaidi ya 60 wanasadikika kupoteza maisha.
Imetolewa na :
Mkurugenzi Mtendaji,
Ofisi ya Habari na Mahusiano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa