Kwa kipindi cha robo ya tatu sasa ya mwaka wa fedha wa 2018/2019, Waheshimiwa Madiwani wa wilaya ya Kyela, wamefanya ziara ya kutembelea ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule zisizopungua 15, wilayani hapa.
Ziara hizi zimefanywa kwa kupitia kamati zao za kudumu, Na katika ziara hizo kwa ujumla wao waheshimiwa Madiwani, wamesisitiza kuongezwa kasi ya ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi kuanza masomo yao kwa wakati.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Hunter Mwakifuna amesema, serikali ya awamu ya tano imetoa kiasi cha shilingi milioni 400,000,000/=,ili kuwezesha wanafunzi kupata elimu bure na yenye ubora zaidi.
Aidha waheshimiwa Madiwani wamegundua kuwa kuna baadhi ya shule zimekuwa hazina taarifa za ujenzi wa awali na wamezitaka shule hizo kuandaa taarifa hizo na kuziwasilisha haraka.
Pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Hunter Mwakifuna, alitoa muongozo wa matumizi ya fedha ambazo zimetolewa na serikali, kwa lengo na kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa malengo kusudiwa tu na si vinginevyo.
Aidha pongezi zimetolewa kwa baadhi ya viongozi wa shule na wenyeviti wa bodi za shule, kwa kusimamia ujenzi wa awali wa maboma mengi ya madarasa. Shule ya sekondari ya Mwaya iliopo Kata ya Mwaya wilayani Kyela ni miongini mwa shule zilizopongezwa na kupewa shilingi milioni 100,000,000/= kwa umaliziaji wa maboma ya madara 9, waliyoyajenga kwa nguvu za wananchi.
Mwisho walimu, viongozi pamoja na wananchi wameipongeza serikali kwa kuwasaidia katika umaliziaji na ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani hapa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa