• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Afisa Elimu Mkoa Wa Mbeya Afanya Kikao Kazi Na Viongozi, Walimu Kyela

Imewekwa Kwenye: July 12th, 2023


Afisa elimu mkoa wa Mbeya ndugu Ernest Hinju, amefanya kikao kazi tarehe 11/07/2023, katika viwanja vya shule ya msingi Nkuyu hapa wilayani Kyela.

Kikao kimeshirikisha Viongozi na walimu, akiwemo Afisa taaluma Mkoa ndugu, Kaniugu, Afisa elimu (W) ndugu, lydia Herbert, Afisa elimu Msingi (W) ndugu, Rowllence B.Kabuje, Maafisa taaluma (W), Maafisa elimu kata, Wakuu wa shule, walimu wakuu, pamoja na walimu wawili mahili wa masomo 6 katika ufundishaji.

Akizungumza katika kikao hicho Afisa elimu Mkoa ndugu Ernest Hinju amesema;

Lengo la kufanya kikao hicho ni kujadiliana mikakati ya kuinua taaluma katika mkoa wetu wa Mbeya, kufanya tathimini ya matokeo ya mtihani wa "MOCK" kanda kwa darasa la saba 2023.

"Ili kupata nafasi ya mkoa au wilaya katika taaluma, hesabu ya matokeo kwa mitihani 5 hufanywa, yaani mtihani wa darasa la 4, 7, kidato cha 2, 4 na 6 ili kupata wastani,  hivyo hutuwezesha kujua nani anashika nafasi ya kwanza, Idara ya Elimu sekondari ni lazima wahusike katika kufanya tathimini ya matokeo" amesema ndugu Ernest Hinju.

Aidha amesema, amekuwa akifanya vikao kazi kwa kila halmashauri za Mkoa wa Mbeya, ili kuweka mikakati ya kupandisha Mkoa kitaaluma.

Pamoja na hayo, amewataka viongozi, walimu kudumisha upendo katika sehemu zao za kazi ili kuweka akili sawa na hatimae kuinua taaluma kwa wanafunzi wanaowafundisha.

Ametoa pongezi kwa Mkoa wa Mbeya kwa kuendelea kushika nafasi ya 3 Kitaifa, na amesisitiza upendo na mshikamano baina ya watumishi kwa lengo la kuinua taaluma ndani ya Mkoa.

"Mkoa wetu wa Mbeya umekuwa ni mfano wa kuigwa katika elimu na usimamiaji mzuri wa miradi kwa mikoa mingi nchini, na hata mikoa mingine imekuja kujifunza kwetu" Amesema Afisa elimu mkoa.

Nae Afisa elimu msingi (W) ndugu, Rowllence B. Kabuje alitoa tathmini ya matokeo ya mtihani wa darasa la 7 "MOCK" kanda, inayoshirikisha mikoa 5, wilaya ya Kyela ikiwa imeshika nafasi ya 18 kati ya halmashauri 27 za kanda.

Ndugu Ernest Hinju ataendelea na ziara za kufanya kikao kama hiki katika halmashauri nyingine za Mkoa wa Mbeya.

Mwisho.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WATAALAM WA AFYA KUTOKA MALAWI WAFANYA KIKAO NA WATAALAM WA AFYA KUTOKA KYELA KUJADILI NAMNA YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO

    July 02, 2025
  • BIDHAA FEKI ZILIZOINGIA KWA NJIA HARAMU ZATEKETEZWA KWA MOTO

    July 01, 2025
  • KYELA YAFANIKISHA UNUNUZI WA GARI JIPYA AINA YA TOYOTA HILUX KUPITIA MAPATO YA NDANI KWA TSH. MILLIONI 149.1

    June 30, 2025
  • SERIKALI YAWAPUNGUZIA WANANCHI ADHA YA ELIMU KWA KUJENGA SHULE KARIBU YAO

    June 27, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa