Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya Kyela wametoa shukrani zao za dhati, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuiwezesha Hospitali ya wilaya ya Kyela, kununua vifaa tiba vya kisasa vyenye thamani ya shilingi 376,000,000/= ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mitambo katika hospitali hiyo.
Shukrani hizi zimetolewa katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo, kwa robo ya 2 ya mwaka 2022/2023. Waheshimiwa madiwani wamesema kwa sasa Hospitali ya wilaya imekuwa na vifaa tiba vya kisasa na vya kutosha kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali bila usumbufu wowote.
Akiongea na waheshimiwa madiwani wa kamati ya Elimu na Afya, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Lembris Leizer amesema,
Baada ya mapokezi ya fedha hizo, Halmashauri iliandaa mahitaji ya kila kitengo katika hospitali ya wilaya, na kununua vifaa kulingana na mahitaji ya kitengo.
"stationary bicycle" mashine ya kuwasaidia waliopata kiharusi na kuleta mzunguko wa damu kwenye mwili, "Microscope olmpus cx23" inayosaidia kutambua wadudu wasioweza kuonekana kwa macho, Mashine za magonjwa yote ya meno, Mafriji kwa ajili ya kutunzia damu, mitambo ya kufulia nguo pamoja na vifaa vingine vingi vimemunuliawa.
Aidha waheshimiwa madiwani kwa kupitia kamati zao za kudumu wameweza kupitia na kukagua miradi ifuatayo;
Kikundi cha wajasiriamali bodaboda kikundi kilichokopeshwa fedha na halmashauri, ujenzi wa vyumba 17 vya madarasa katika shule ya sekondari Mwakilima, shule ya msingi uhuru, shule ya sekondari Kafundo, shule ya msingi Ikulu, pamoja na shule ya sekondari Lubele.
Ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari Kyela coal mine.
pamoja na miradi hiyo kamati hizo zimeweza kutembelea ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya Kyela coal mine, ujenzi wa kituo cha afya kata ya Itope, ujenzi wa zahanati ya Itekenya katika kata ya katumba songwe, ujenzi wa shule mpya ya sekondari Ibanda, ikiwa ni pamoja na jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya Njisi.
Ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari Nyasa lakeshore.
Aidha katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri Katule G. kingamkono alijitolea kuwa mlezi wa Jackline Mshana na kuahidi kumlipia bima ya NHIF mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu, katika shule ya msingi Isaki,
Hata hivyo Mhe. Mwenyekiti ameahidi kutoa mifuko 30 ikiwa mifuko 10 kwa ujenzi wa Shule mpya ya ibanda, mifuko 10 kwa ujenzi wa kituo cha Afya Itope na mifuko 10 kwa ujenzi wa zahanati ya Itekenya. Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi aliahidi kupeleka mifuko 10 ya simenti katika ujenzi wa zahanati ya Itekenya kwa niaba ya wataalam.
Mwisho pongezi nyingi zimetolewa kwa wataalam kwa kusimamia na kutekeleza vyema maagizo yanayotolewa na viongozi na hata kuifanya miradi mingi ya maendeleo kukamilika kwa wakati na viwango vikubwa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa