Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, wamefanya Baraza la kazi la robo ya kwanza leo 30/10/2023, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Baraza hilo limehudhuriwa na waheshimiwa madiwani wote, Mkuu wa wilaya Mhe. Josephine Manase, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Wakuu wa Idara mbalimbali na Vitengo.
Akifungua baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono amewasifu wataalamu kwa kufanya kazi vizuri kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah A. Luhala, amezipokea pongezi hizo kwa dhati na kuahidi kuendelea kuchapa kazi.
Katika Baraza hilo waheshimiwa Madiwani wamepata nafasi ya kuwasilisha taarifa za kazi kutoka katika kata zao.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa