Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, wamefanya Baraza la kazi la robo ya pili leo 15/03/2024, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Baraza hilo limehudhuriwa na waheshimiwa madiwani wote, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Wakuu wa Idara mbalimbali na Vitengo.
Akifungua baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono amewasifu wataalamu kwa kufanya kazi vizuri kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Pia ametumia nafasi hiyo kukabidhi fedha za mchango kutoka kwa Baraza la Waheshimiwa Madiwani kiasi cha shilingi 400,000/= kwa mwenyekiti wa kamati ya kuchangisha michango ya kuwasaidia wazee kupata bima, ambae ni Mkurugenzi Mtendaji Bi. Florah Ruhala.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah A. Luhala, amezipokea pongezi hizo kwa dhati na kuahidi kuendelea kuchapa kazi.
Katika Baraza hilo waheshimiwa Madiwani wamepata nafasi ya kuwasilisha taarifa za kazi kutoka katika kata zao ikiwa ni pamoja na taarifa ya ukusanyaji wa mapato.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa