• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DC MANASE AZINDUA RASMI ZOEZI LA UGAWAJI WA KADI ZA BIMA YA AFYA KWA WOTE KWA KAYA ZISIZO NA UWEZO (ZINAZOHUDUMIWA NA MPANGO WA TASAF)

Imewekwa Kwenye: February 9th, 2026

Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mhe. Josephine Manase, tarehe 09 Februari 2026 amezindua rasmi zoezi la ugawaji wa Kadi za Bima ya Afya kwa Wote kwa kaya maskini katika hafla iliyofanyika Kata ya Bondeni, wilayani Kyela.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Manase amesema kuwa awamu ya kwanza ya zoezi hilo inalenga kuandikisha kaya maskini, ambapo walengwa watasajiliwa na kupatiwa vitambulisho vya bima ya afya vitakavyowawezesha kupata huduma za matibabu kwa kipindi cha mwaka mzima bila gharama yoyote. Amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imechukua jukumu la kugharamia bima hizo ili kuhakikisha wananchi wenye uhitaji wanapata huduma za afya bila vikwazo vya kifedha.

Ameeleza kuwa katika awamu ya kwanza, jumla ya walengwa 6,731 sawa na Kaya 1881 watafikiwa katika kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, kwa lengo la kuwaandikisha na kuwawezesha kunufaika na huduma za bima ya afya. Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote.

Aidha, Mhe. Manase amewataka wananchi wa Kata ya Bondeni kuwa mabalozi wa kuhamasisha wenzao kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo, akisisitiza kuwa fursa hiyo ni muhimu kwa ustawi wa afya za familia na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Adv. Florah A. Luhala, amewataka wananchi waliopata kadi hizo kuzitunza na kuzitumia kwa matumizi sahihi, akionya dhidi ya kuzitoa kwa watu wengine kwani kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu za matumizi ya bima ya afya.

Kwa niaba ya Wananchi wa Kata ya Bondeni, Bi. Victoria Mwaitenda, amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea wananchi mpango huo muhimu, akisema umewaletea matumaini mapya ya kupata matibabu bila hofu ya gharama. Amesema hatua hiyo itaondoa adha kubwa iliyokuwa ikiikumba familia nyingi zenye kipato cha chini.

Ikumbukwe kuwa zoezi la uandikishaji wa Bima ya Afya kwa Wote ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali unaolenga kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma za afya kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa bima ya afya, hatua inayochochea ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DC MANASE AZINDUA RASMI ZOEZI LA UGAWAJI WA KADI ZA BIMA YA AFYA KWA WOTE KWA KAYA ZISIZO NA UWEZO (ZINAZOHUDUMIWA NA MPANGO WA TASAF)

    February 09, 2026
  • BARAZA LA MADIWANI LAPOKEA KWA SHANGWE TAARIFA YA MHE. DC KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE NAKUAHIDI KWENDA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    February 09, 2026
  • MILIONI 570 ZATOLEWA KWA VIKUNDI VYA VIJANA, WANAWAKE PAMOJA NA WATU WENYE ULEMAVU

    January 07, 2026
  • MKURUGENZI MTENDAJI KYELA ADV. FLORAH A. LUHALA AWATAKA WATUMISHI WAPYA 50 KULINDA NIDHAMU YA KAZI NA KUHUDUMIA WANANCHI

    December 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa