• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri Ya wilaya Ya Kyela Yaungana Na Wadau Wa Mazingira Katika Kufanya Usafi Hapa Wilayani

Imewekwa Kwenye: April 19th, 2023

Wataalam wa Afya, Maendeleo ya jamii na Mazingira kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa kushirikiana na Barozi wa mazingira Ndugu Nestory Mushi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Asasi zinazojishughulisha na usafi wa Mazingira IECA kutoka Ileje, EMEDO, ARENA RECYCLING kutoka Jiji la Mwanza, Wamefanya usafi wa mazingira  katika  kata mbalimbali za Wilaya ya Kyela.

Kata ya Matema, kata ya Njisi, Kata ya Mikoroshini ni mojawapo wa kata zilizopitiwa na zoezi hilo lililoanza kuanzia tarehe 17/04/2023 na litahitimishwa tarehe 19/04/2023 kwa kufanya usafi katika kata ya Mwanganyanga.

Akitoa elimu ya usafi wa mazingira kwa wananchi wa kata ya Mikoroshini Mhadhiri msaidizi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Ndugu Bahati Mayoma amesema, taka zote hizi zimeundwa na kemikali mbalimbali ambazo si rafiki kwa afya ya binadamu.

Hivyo lengo la kufanya usafi huu ni pamoja na kutoa Elimu ya kuepuka jinsi ya kutotumia  bidhaa za plastiki pale inapowezekana.

Aidha amewataka wananchi kudhibiti taka kutoka katika makazi yetu ili kuisaidia Serikali kutotumia gharama kubwa kuondoa taka mtaani, na badala yake tunaweza kuzitunza taka hizo, hasa zile za plastiki na kuzigeuza kuwa fulsa ya kutengeneza bidhaa mpya.

"Tunafanya usafi huu pamoja na kutafiti ni aina gani za taka ambazo zinachafua mazingira kwa kiasi kikubwa kisha tutakuja na majibu kwa serikali na utatuzi wa tatizo la taka hizo kwa wananchi" amesema Mayoma.

Pamoja na hayo ndugu Mayoma amesema, kwa hapa Tanzania tafiti kadhaa zimeonesha kuwa taka za plastiki ikiwemo nyavu zilizotelekewa zimetapakaa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fukwe za Bahari, Maziwa na Mito ambapo baadhi ya viumbe wakiwemo samaki, vimethibitika kuwa na vipande vidogo vidogo vya plastiki (microplastics) katika matumbo yao.

Kadhalika taka za plastiki zimethibitika kuwa chanzo cha kuenea kwa vimelea vinavyoweza kupelekea usugu wa dawa (AMR) n.k.  Kwa upande wa nyavu zilizotelekezwa, zimeendelea kuzonga na kunasa samaki bila uangalizi wa binadamu (Ghost fishing).

Hali hii siyo tu inatishia uendelevu wa sekta ya uvuvi, uchumi wa jamii, na usalama wa chakula kitokanacho na protini ya samaki ambayo hutegemewa zaidi na jamii inayozunguka maziwa makuu pamoja na Bahari, bali pia taka hizi zinadhoofisha malengo mtambuka ya mchango chanya unaotakana na uchumi wa bluu pamoja na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Zoezi bado linaendelea hadi tarehe 20/04/2023.

Mwisho.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa