• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kamati Ya Siasa Ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa Wa Mbeya Yakagua Miradi Ya Maendeleo Kyela

Imewekwa Kwenye: March 19th, 2022

Mheshimiwa James Mwampondele (kofia ya njano kulia) kwa niaba ya Mheahimiwa mwenyekiti wa kamati ya siasa mkoa wa Mbeya, akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa na kamati ya siasa ya wilaya, wakiwa  katika mradi wa ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Kyela.

Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo wilayani Kyela, ziara iliyofanyika kuanzia tarehe 18/03/20222 hadi tarehe 19/03/2022.

Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na kamati hiyo ni pamoja na miradi ya ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Kyela, Kikundi kinachojishughulisha na utengenezaji wa viungo vya chakula, mradi wa utengenezaji wa makaravati 6 ya barabara ya Kamanga-Lusungo, mradi wa umeme katika kijiji cha Kingili kata ya Ipinda.

Mradi wa one stop boder post katika kata ya Njisi, mradi wa ujenzi wa wodi ya mama na mtoto pamoja na maabara katika zahanati ya  Kilasilo kata ya Ikimba, ujenzi wa taa za barabarani katika kata ya Ipinda ujenzi wa barabaraya rami njia panda ya Busale, Kikundi cha Bodaboda katika kata ya Ipinda pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara za rami Kyela mjini.

Kamati ya siasa ya Mkoa wa Mbeya wakiwa katika Kikundi cha bodaboda katika kata ya Ipinda Kyela.

Akiwa katika ujenzi wa wodi ya mama na mtoto, Mwenyekiti wa kamati ya wazazi CCM Mkoa Mheshimiwa James Mwampondele, Alitoa ushauri kwamba, wataalam wafanye tathmini ya kiwango cha gharama ambazo zinaweza kumaliza jengo hilo, ili chama kinaposukuma upatikanaji wa fedha kupatikana basi wasukume pesa ile tu ambayo imekwama katika kunalizia mradi huu wa jengo la mama na mtoto.

Pamoja na hayo Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya Dr. Mariam Ngwere aliwatoa hofu wanakamati kwa kuwaambia kuwa vifaa vya ujenzi wa hatua inayofuata kwa ujenzi vyote vipo stoo.

Aidha ziara haikuishia hapo, kamati ilifika hadi katika kikundi cha Mkami Group ambapo Mwenyekiti wa kamati ya wazazi CCM Mkoa alipata wasaa wa kuongea na wanakikundi hicho na  kuwapongeza kwa kazi wanazozozifanya na kuwaahidi kutatua baadhi ya changamoto wanakabiliana nazo.

Kamati ya siasa mkoa ikiwa katika picha ya pamoja na kikundi cha MKAMI GROUP hapa wilayani Kyela.

Akiwa katika mradi wa REA katika kijiji cha Kingingili kata ya Ipinda, Mheshimiwa Mwenyekiti, aliuagiza uongozi wa TANESCO Kyela kutengeneza Mpango kazi na kuuwasilisha katika chama ngazi ya wilaya na mkoa, ili viongozi wapate kujua nini cha kuzungumza kwa wananchi juu ya huduma za umeme zinaziendelea kutolewa kwa wanachi.

Mwisho kamati ilifurahishwa sana na umoja uliopo Kyela hasa kwa viongozi wa chama na serikali na hata kuwezesha miradi mingi ya maendeleo kuibuliwa na kutekelezwa wilayani hapa.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa