Wananchi wa kata ya Busale kijiji cha Busoka wafurahia kupata zahanati,
Pia wametoa shukrani zao za thati kwa serikali ya awamu ya sita, kwani Serikali imewaletea zaidi ya shilingi milioni 75 ili kuwasaidia katika ujenzi wa zahanati hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa kijiji cha Busoka ndugu Said James amesema, ikikamilika zahanati itahudumia zaidi ya wananchi 1000, hivyo kuwa msaada mkubwa kwa wananchi wao na kuepukana kufuata huduma ya afya umbali mrefu.
Hadi sasa ujenzi wa zahanati hiyo upo katika hatua ya upauaji.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa