• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kyela Polytechnic College Yafungua Mafunzo Ya Ufundi Kwa Wanafunzi 337

Imewekwa Kwenye: June 25th, 2021


Chuo cha mafunzo ya ufundi Kyela Politechnic collage (KPC), Kimefungua mafunzo ya ufundi kwa wanafunzi 337, ambao wamelipiwa ada na ya mafunzo hayo na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, mafunzo yatakayofanyika kwa miezi sita. Mafunzo hayo yamefunguliwa leo tarehe 25/06/2021, katika viwanja vya chuo hicho hapa wilayani Kyela. 

Akifungua mafunzo hayo Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri Katule G. Kingamkono, amewataka wanafunzi hao kusoma kwa jitihada na kuachana na mambo ya mtaani. Pia Mheshimiwa mwenyekiti aliwakumbusha wanafunzi hao kuwejiwekea malengo tangu wanapoanza masomo yao hadi watakapomaliza, ili elimu watakayoipata, ikawasaidie wao katika kujiajiri na kusaidia jamii kwa ujumla. 

Pamoja na hayo Mheshimiwa mwenyekiti amemhadi Mkuu wa chuo hicho kwamba, atatoa mikopo kwa vikundi 2, ambavyo vitaundwa na vijana hao punde baada ya kumaliza masomo yao, hii ni kwasababu ya kuwatia moyo vijana hao na kuongeza jitihada katika swala zima la kujiajiri.

Aidha Mkuu wa Chuo hicho ndugu Salatiel Mwakiambiki, aliwaasa wanafunzi hao kwa kusema, utajiri si lazima mtu aje akuwekee pesa mfukoni, bali hata kwa kutumia fulsa kama hii ambayo serikali imejitolea, kuwalipia wanafunzi ada hii, ambayo itawasaidia kusoma na baadae kwenda kujiajiri. Pia aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa na upendo kwa wenzao ambao wamekosa nafasi hii, kwani kwa kufanya kwao vizuri anaamini, kwa awamu nyingine serikali itaongeza idadi ya wanafunzi hivyo hata wale waliokosa nafasi kwa sasa wataweza kufaidika. 

Nae Makamu Mkuu wa chuo hicho bi. Upendo Mwinuka amesema wanafunzi hao watafundishwa elimu ya vitendo kwa 60% na baada ya hapo watatafutiwa maeneo mbalimbali ili waweze kufanya mazoezi kwa vitendo zaidi na kuwa  tayari kwa kujiari. 

Kwa upande wao wanafunzi wametoa pongezi kwa serikali yao, kwa kuwalipia ada ili wao waweze kupata elimu hiyo itakayoweza kwasaidia wao kujiajiri, na baadae kuisadia jamii ya Wana Kyela na watanzania kwa ujumla. 

Sherehe hizi zilihuzuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi ndugu Raphael Samweli, Mheshimiwa diwani wa kata ya Ndandalo Kefa Mwanganda, Afisa tarafa ya Unyakyusa ndugu Herry Willium pamoja na katibu wa Mbunge ndugu Edgar Mwasamlaghila. 

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa