Mbunge wa jimbo la Kyela Mhe. Ally Mlaghila Jumbe akiongozana na Mkuu wa wilaya Mhe. Josephine Manase, wamepokea mabomba ya utekelezaji mradi wa maji wa Ngana.
Mabomba yamepokelewa tarehe 13/07/2023 katika eneo la chanzo cha maji mto Mwega ikiwa ni hatua ya awali ya mapokezi ya mabomba ya mradi wa maji Ngana.
Aidha Mheshimiwa Ally Mlaghila Jumbe(MB) na Mhe. Josephine Manase wametoa shukrani zao za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka wanaKyela kwa mradi wa maji ambao unakwenda kupunguza kero ya maji kwa wananchi.
Mradi wa maji wa Ngana utatumia shilingi 7,999,386,700/= na unategemewa kumalizika mwezi Novemba 2023.
Mradi utakapo kamilika unategemewa kuhudumia wananchi wa kata ya Nagana, Ikimba, KatumbaSongwe, Ikolo, Ngonga pamoja na Bujonde ambapo kata hizo zinatakribani wakazi efu 62.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa