Mamlaka ya Mji mdogo wa Kyela imezidi kupaa kimapato kuanzia robo ya kuanzia julai 1 mwaka 2021 hadi kufikia mwezi juni 30/2022, kwa kukusanya jumla ya shilingi 387,545, 723/= ikiwa ni sawa na asilimia 96 ya makisio ya bajeti ya mwaka 2021/2022 ya shilingi 402,173,000/= kiwango ambacho hakijawahi fikiwa tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo.
Akitoa taarifa katika Baraza la mwaka la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kyela lililofanyika katika ukumbi wa Mamlaka hiyo tarehe 23/09/2022, Mwenyekiti wa Mamlaka Mheshimiwa Emmanuel K. Bongo amesema;
Mamlaka ya Mji Mdogo Wa Kyela umefanikiwa kuchangia 10,000,000/= katika ujenzi wa zahanati ya Ndandalo, kuchangia mchanga katika ujenzi wa kituo cha Afya cha Itunge kituo kilichojengwa kwa fedha za tozo, uchangiaji wa shilingi 38,754,572.30 kwa ajiri ya ukopeshaji wa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambayo ni sawa na asilimia 100 ya uchangiaji.
Aidha amesema, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kyela imefanikiwa kujenga vibanda 10 vya biashara katika stendi kuu ya mabasi hapa Kyela mjini. Pia Mamlaka ya Mji mdogo Kyela imetenga fedha shilingi 68,000,000/= kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, amabapo shilingi 30,000,000/= zimetengwa kwa ajiri ya ukarabati wa stendi ya mabasi hapa Kyela mjini, Shilingi 15,000,000/= zimetengwa kwaajili ya ukarabati wa choo cha stendi, shilingi 20,000,000/= zimetengwa kwa ajiri ya kukarabati soko la olofea na shilingi 3,000,000/= zimetengwa kwa ajiri ya kuchangia ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi Mbugani, Uhuru na Nkuyu.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Bongo ametoa shukrani zake za dhati kwa ushikiano mkubwa uliopo baina ya Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Ismail Mlawa, Mbunge wa jimbo la Kyela Mhe ally Mlaghila Jumbe, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Katule G. Kingamkono, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Ndg. Ezekiel H. Magehema
pamoja na wataalam wote bila kumsahau mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Ndugu Gerald Mlelwa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuongeza mapato katika Mamlaka hiyo.
Mwisho Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kyela Ndugu Gerald Mlelwa amesema; mafanikio yote yanayoonekana katika Mamlaka ni mchanganyiko wa juhudi kubwa za ushirikiano zinazofanywa na viongozi waliopo katika wilaya ya Kyela lakini pia ushirikiano mkubwa uliopo baina ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kyela na Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa