• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mhe. Mkuu Wa Wilaya Ya Kyela Aendelea Na Ziara Ya Kusikiliza Kero Kwa Wananchi

Imewekwa Kwenye: June 4th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe, Josephine Manase amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Muungano kijiji cha Bukinga na Lutusyo tarehe 3/6/2024.

Katika ziara yake  Mhe, Mkuu wa Wilaya ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, baadhi ya wakuu wa idara na vitengo, na wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali .

Akizungumza na Wananchi wa kata hiyo  Mhe, Josephine Manase ameomba wananchi  kuwa wazalendo kufanya shughuli za maendeleo, amepongeza uongozi wa zahanati ya kijiji cha Bukinga kata ya Muungano kwa kutoa huduma bora za afya na kupunguza kero za wanachi.

"Leo hii Mganga mfawadhi wa zahanati ya ya kijiji cha Bukinga umesifiwa na wananchi kwa utoaji mzuri wa huduma za afya kwa wananchi hawa, hivyo kazana kufanya kazi, maana Mgema akisifiwa Tembo hutia maji, itakuwa si vizuri ukajisahau kufanya kazi kwa sifa ulizopata, hongera kwa kutimiza majukumu yako". amesema Mhe. Manase.

Wananchi, wametoa kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na  changamoto ya umeme ,maji, ujenzi wa  Zahanati , uhaba  wa  watumishi kwa  upande wa  elimu na afya, ujenzi wa soko, ubovu wa miundombinu na ushuru kwa wakulima wa mpunga.

Baadhi ya kero hizo zipatiwa majibu na nyingine zimechukuliwa kwa ajili ya kuzinafanyiwa kazi.

Aidha ameomba wanafunzi waliohitimu kwa taaluma mbalimbali kutumia mifumo  yakiserikali inayohusika kutoa ajira, ili kufanya maombi ya ajira kutokana na taaluma zao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi   mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Dkt. Saumu Kumbisaga amewaomba wananchi kuwachagua wazee wasiojiweza wenye  umri zaidi ya Miaka 60, kupitia mikutano yao ya kata ili waweze kupata huduma za afya bure, ikiwa ni sambamba na wajawazito, watoto chini ya miaka 5, kama isemavyo sera ya Afya.

Nae Afisa uhamiaji wilaya Kyela Vitales Komanya ameomba wananchi wa kata  hiyo  kufuata utaratibu maalumu wa kupokea wageni ili kuepukana  na matendo ya uhalifu pia kulinda amani na usalama kuelekea kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa, na amewasisitiza wananchi wa kata ya Muungano kupata vitambulisho vya taifa ikiwa ni kampeni ya  "mjue jirani yako".

Aidha Mhe, MKuu wa wilaya amewaomba viongozi wa kijiji  na Wananchi kuunda kamati ya ulinzi shirikishi ili kuepukana na matendo uhalifu , pia  ameomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuboresha taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura.

Sambamba na hayo Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Kyela, amemaliza kwa kuwaomba wananchi kutunza mazingira ili kuepukana na hali ya majangwa kupitia athari za ukataji miti hovyo  ikiwa ni kuendeleza kauli mbiu ya "Matumizi ya nishati Safi" ya  Mheshmiwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mwisho.....

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa