• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mhe. Mkuu Wa Wilaya Ya Kyela Akutana Na Wananchi Wa Kata Ya Ipande Na Kusikiliza Kero Zao

Imewekwa Kwenye: July 6th, 2024

Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase ametembelea kata ya Ipande kijiji cha Njugiro, akiendelea na ziara yake ya kusikiliza kero mbalimbali zinazo wakabili wananchi katika wilaya ya Kyela.

Katika ziara hiyo iliyofanyika tarehe 05/07/2024, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amefurahishwa wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutoa kero zao.

Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela, amefanikiwa kutoa suluhisho wa kero mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wananchi wa kata ya Ipande, ambapo wananchi walitoa kero mbalimbali zinazowasumbua ikiwemo suala la afya, Elimu, Kilimo pamoja na Umeme.

Kuhusu suala la Ukosefu wa zahanati, Mhe. Josephine Manase ameahidi kutoa kiasi cha Tsh. 200,000 kama chachu, kwaajili ya kuhamasisha mchakato wa kuanza ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho cha Njugiro.

Kuhusiana na suala la umeme kupatikana maeneo ya masoko, na shuleni katika kijiji hicho, Mratibu wa umeme wa "REA"  Ndugu. Jairo Simion Sichura amewatoa hofu wakazi wakijiji hicho cha Njugiro kuwa katika mwaka mpya wa fedha Serikali imetenga bajeti kubwa ambapo mpaka kufikia mwakani vijiji vingi vitapata umeme na kijiji cha Njugiro kitapewa Kipaumbele.

Pamoja na hayo Mkuu wa wilaya ya Kyela ameumizwa na ukosefu wa daraja lililosombwa na maji, daraja ambalo lilikuwa lina unganisha kitongoji cha Kipela na Njugiro ambapo limeleta adha ya mawasiliano baina ya vitongoji hivyo viwili, pia limesababisha kukosekana kwa baadhi ya huduma za kijamii.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amewaahidi wananchi hao kuwa, anaenda kulifanyia kazi suala hilo na atarudi na suluhisho mara moja.

"Kumekua na mazoea mabaya ya vijana wa Bodaboda kuendesha Pikipiki mpaka kwenye Madaraja ya kamba (viteputepu) ambapo wanaharibu mbao za madaraja hayo" alisema Mhe. Josephine Manase.

Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kyela (OCD) Ndug. Lwitiko Mwanjala amewaasa vijana wa Bodaboda kuzingatia sheria za Barabarani kwa manufaa yao wenyewe na familia zao.

Mwisho Mhe. Josephine Manase amehitimisha ziara hiyo kwa kuwataka wananchi wa kata ya Ipande kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi bora kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa. Pamoja na kushirikiana katika kupiga vita mimba za utotoni.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WATAALAM WA AFYA KUTOKA MALAWI WAFANYA KIKAO NA WATAALAM WA AFYA KUTOKA KYELA KUJADILI NAMNA YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO

    July 02, 2025
  • BIDHAA FEKI ZILIZOINGIA KWA NJIA HARAMU ZATEKETEZWA KWA MOTO

    July 01, 2025
  • KYELA YAFANIKISHA UNUNUZI WA GARI JIPYA AINA YA TOYOTA HILUX KUPITIA MAPATO YA NDANI KWA TSH. MILLIONI 149.1

    June 30, 2025
  • SERIKALI YAWAPUNGUZIA WANANCHI ADHA YA ELIMU KWA KUJENGA SHULE KARIBU YAO

    June 27, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa