Wazee maarufu na wastaafu wakiwa wamejipanga katika kuanza mdahalo katika ukumbi wa Halamashauri wilayani Kyela. Ikiwa ni maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru Tanzania Bara.
Maadhimisho ya ya siku 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara yameashimishwa kwa kishindo hapa wilayani Kyela, maadhimisho haya yalianza kuadhimishwa kuanzia tarehe 01/12/2022 hadi kufika kilele tarehe 09/12/ 2022.
Katika wilaya ya Kyela maadhimisho haya yameshirikisha wananchi kwa kufanya usafi wa mazingira, Mahojiano mbalimbali yaliyohusu maendeleo Nchi kabla na baada ya uhuru, upandaji wa miti katika mazingara, Michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji wa zawadi kwa washidi wa michezo, Na kuhitimishwa kwa kupitia Mdahalo mkubwa uliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela tarehe 09/12/2022.
Akitoa hotuba yake Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa SACP. Ismail Mlawa amesema, wilaya ya Kyela ni wilaya iliyozaliwa kutoka katika wilaya ya Rungwe mwaka 1972, baada ya uhuru wa Tanzania Bara na kuanza kujitegemea katika nyanja mabalimbali za kimaendeleo.
Amesema wilaya ya Kyela miaka 61 ya Uhuru imeweza kufanya maendeleo mengi sana kwa wananchi wake katika secta zote muhimu ikiwemo, Kilimo, Afya Elimu pamoja na miundo mbinu.
Akizungumzia suala la elimu Mheshimiwa Ismail amesema, kabla ya uhuru Kyela ilikuwa na shule za msingi 18 tu, lakini baada ya miaka 61 ya uhuru Kyela inashule 112 za msingi maendeleo yaliyopatika kwa kasi ya ajabu.
Kwa upande wa afya Mheshimiwa Mkuu Mkuu wa wilaya amesema, wilaya ya Kyela kabla ya uhuru ilibahatika kuwa na kituo cha Afya 1 ambapo kwa sasa ndiyo hospitali ya wilaya, ila baada ya Uhuru Kyela imekuwa na Hospitali 3, vituo vya afya 5 zahati 41pamoja na cliniki10.
Aidha aliendelea amesema kwa upande wa miindo mbinu wilaya ya Kyela imepiga hatua kubwa kwa kutengeneza barabara za lami zenye kilometa 56.8, barabara za changalawe kilometa 75.6 pamoja na barabara za udongo kwa kilometa 435.19 kiwango ambacho huwezi fananisha kabla ya miaka 61 ya Uhuru.
Suala la umeme Mheshimiwa malawa amesema, wilaya ya Kyela kwa sasa imefanikiwa kuwa na umeme wa uhakika na wilaya imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme kwa kata zote 33, vijiji 58 pamoja na vitongoji 176 katika wilaya ambapo kabla ya uhuru huduma ya umeme haikuwa ya uhakika katika wilaya.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa