Mashindano ya Samia Nanenane Pre Season League 2023, yamefunguliwa leo tarehe 27/07/2023 wilayani Kyela katika viwanja vya Kipija Arena na viwanja vya Mwakangale.
Akifungua mashindano katika viwanja vya Kipija Arena, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera amesema;
Michuano hii imeanzishwa kwa lengo la kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani, ambae amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo, hususani mpira wa miguu, ambapo katika mashindano ya ligi kuu Tanzania, alitoa shilingi milioni 5 hadi 20 ili kuongeza hamasa kwa wachezaji kupata ushindi.
Amesema, Viongozi wa Mikoa wameamua kufanya mashindano hayo kwa kutambua mchango alionao Mhe. Rais wa kupenda michezo.
"Nimekuja katika mashindano haya nikiwa na jenzi ambazo zimetolewa na wadhamini, nitazigawa jenzi kwa timu zote hadi timu za wageni zitapata".
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amekitaka chama cha mpira Kyela, kujitathimini na kuhakikisha kufikia mwakani lazima wawe na timu ambayo itakuwa inashiriki daraja la 2 au la 3, kama kitashindwa basi viongozi ni heki wakee pembeni kuwapisha watakoweza kuinua timu kutoka wilaya ya Kyela.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Kyela, amemshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa mbeya kwa kuleta mashino ya mpira wilayani Kyela, kwani yanaongeza hamasa kwa wananchi kuipenda michezo.
Nae Mbunge wa jimbo la Kyela Mhe. Ally Mlaghila Jumbe, amempongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kuipenda wilaya ya Kyela na kuleta mashindano ya Samia Nanenane Pre season league 2023, Pia ametoa shukrani zake za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kuipa miradi mingi ya maendeleo wilaya ya Kyela. Amesema pamoja na hayo bado Mhe. Rais ametupa shilingi bilioni 3 ambazo zinajenga shule ya wasuchana ya mkoa katika kata ya Busale.
Awali Afisa Michezo wa Mkoa ndugu Mfugale alizitaja timu zinazoshiriki mashindano hayo kuwa ni pamoja na timu ya Mbeya City, Ken Gold, Nakonde Tc kutoka Zambia, Tanzania Prison, Ihefu, Mbeya kwanza, Rungwe Dc, Chunya Dc, Mbarali Dc, Timu 2 kutoka Malawi pamoja na bingwa Mtetezi Kyela Dc.
Finali za mashindano hayo inatarajiwa kufanyika tarehe 02/08/2023.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa