Akizungumza na Maafisa ugani wa wilaya ya Kyela, katika semina ya mafunzo ya matumizi ya mbolea aina ya YALA, iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Kyela tarehe 12/12/2019. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, ndugu Ezekiel Magehema amesema;
Katika uongozi wake atahakikisha kuwa kila afisa ugani alieajiriwa katika Halmashauri hii, anaishi katika maeneo ya kituo cha kazi yake. Hii ni katika kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma sahihi ya kilimo.
Pia ndugu Magehema amewahakikishia maafisa ugani hao, kuwa na moyo wa kufanya kazi katika maeneo waliyopangiwa kwani, serikali ya awamu ya tano ipo katika kupambana na kuhakikisha miundo mbinu, inarekebishwa vizuri na kuwafanya maafisa hao, kufanya kazi bila wasiwasi yoyote.
Mwisho aliwataka maafisa hao kusikiliza kwa makini elimu hiyo ili wakaifikishe vizuri kwa wakulima husika.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa