Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel Magehema amewapokea na kuwapa semina elekezi watumishi wapya 54, wa Idara ya Msingi, Idara ya Sekondari na Idara ya Afya. Mafunzo yaliyofanyika leo tarehe 10/08/2021 katika ukumbi wa shule ya sekondari Kyela Day.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo kazini, ndugu Magehema amewataka, watumishi hao kufanya kazi kwa moyo ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Pia amewaasa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria ,taratibu na miongozo yote ya kazi, katika vituo vyao vya kazi, pamoja na hayo amewaasa watumishi hao kutosahau familia zao walizoziacha nyumbani, na wajitahidi kutunza afya zao.
Mwisho aliwataka Idara, kuwahudumia watumishi wote ambao wataripoti katika vituo vyao, ili kuwaondoa fikra za mawazo mabaya wakiwa kazini.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa