• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu Wa Mkoa Wa Mbeya Afungua Rasmi Mashindano Ya Mbeya Super Cup Wilayani Kyela

Imewekwa Kwenye: July 15th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera amefungua rasmi mashindano ya mpira yajulikanayo kama "Mbeya Super Cup" mashindano yanayoshirikisha timu za mpira kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mbeya, Pamoja na timu kutoa Nchi jirani yaani Zambia, mashindano haya yamefunguliwa tarehe 15/07/2022 katika viwanja vya Mwakangale Hapa wilayani Kyela.

Akifungua mashindano hayo Mheshimiwa Mkuu wa mkoa amesema, kazi ya kuandaa mashindano ya ligi ya mpira, lengo lake kubwa ni kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, pia kuongeza ajira kwa vijana, amesema mashindano kama haya yanatakuwa kufanyika kwa kila mkoa na kwa mkoa wa Mbeya tayari tumekwisha anza kutimiza ilani ya Chama Tawala.

Aidha ametumia fulsa hiyo kutangaza zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi ya mshindi wa kwanza na mshindi wa pili, kupata fulsa ya kushiriki mashibdani ya "Mchele pre-season" katika wilaya ya Mbarali.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Mkuu wa mkoa amesema, kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Mbeya Super Cup atapata fedha taslimu shilingi milioni 7 na kombe lenye thamani ya shilingi laki 7, mshindi wa pili atapata shilingi milioni 5 na mshindi wa tatu atapata shilingi milioni 3, bila kusahau zawadi za makocha bora ikiwa ni pamoja na wafungaji na wachezaji bora, watapewa zawadi zao kwa kiwango kisichopungua 100,000/= 

Nae Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mheshimiwa Dormohamed Issa Rahmat ametoa shukrani zake za dhati kwa Mheshimiwa Mkuu wa mkoa kwa kuanzisha mashindano haya, kwani mashindano haya huibua ajira kwa vijana wengi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Ismail Mlawa, amemshukuru Rais wa awamu ya sita Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mashindano haya kufanyika ndani ya wilaya ya Kyela, kwani mashindano haya yameichangamsha wilaya yetu ya Kyela.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel Magehema, alimpongeza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kwa kuyaleta mashindano haya katika wilaya ya Kyela, na kuahidi kwamba wageni wote waliofika katika wilaya yetu kushiriki michezo hii, watakuwa salama.

Mwisho.


Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • BIDHAA FEKI ZILIZOINGIA KWA NJIA HARAMU ZATEKETEZWA KWA MOTO

    July 01, 2025
  • KYELA YAFANIKISHA UNUNUZI WA GARI JIPYA AINA YA TOYOTA HILUX KUPITIA MAPATO YA NDANI KWA TSH. MILLIONI 149.1

    June 30, 2025
  • KYELA YAFANIKISHA UNUNUZI WA GARI JIPYA AINA YA TOYOTA HILUX KUPITIA MAPATO YA NDANI KWA TSH. MILLIONI 149.1

    June 30, 2025
  • KYELA YAFANIKISHA UNUNUZI WA GARI JIPYA AINA YA TOYOTA HILUX KUPITIA MAPATO YA NDANI KWA TSH. MILLIONI 149.1

    June 30, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa