• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu Wa Mkoa Wa Mbeya Ashangazwa Uwezo Wa Timu Nzuri Za Mpira Zilizopo Wilayani Kyela

Imewekwa Kwenye: August 11th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera ameshangazwa na uwepo na timu za mpira ambazo zinauwezo mkubwa wa kucheza mpira zilizopo wilayani Kyela hadi kuwa tishio kwa timu kubwa.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameyasema haya tarehe 10/08/2022, wakati akifunga mashindano aliyoyaandaa mwenyewe yakitambulika kwa jina la Mbeya Pre season Samia Cup, mashindano yaliyofanyika wilayani Kyela yakishirikisha timu za Ihefu Fc, Kyela Combine, Can Gold, Tanzania Prison, Mbeya city pamoja na Rungwe Dc.

Akiongea kabla ya kufunga mashindano hayo, Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Juma Homera amesema, wilaya ya Kyela ina timu nzuri sana za mpira ila wananchi wameshindwa kuzisaidia timu hizo ili ziweze kufika mbali. Amesema ili kuzisaidia timu hizo atafanya mazungumzo na Mbunge wa jimbo la Kyela ndugu Ally Kinanase, kwa pamoja waweze kuinua timu moja ya mpira wilayani Kyela ili iweze kufika ngazi ya ligi kuu.

Aidha amewataka wananchi wa wilaya ya Kyela kuwa na muamko wa kuzisaidia timu za Kyela kwani timu hizi zimekuwa na uwezo mkubwa katika kucheza mpira lakini zimekosa usaidizi na kufa ikiwemo timu nzuri ya Boma Fc ambayo ilikufa baada ya kukosa usaidizi.

Hata hivyo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi kwa viongozi wote ambao wameziwezesha timu shiriki, kushiriki mashindano hayo kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mashindano, aidha amesema lengo kubwa la mashindano haya ni kutaka kufanya maandalizi kwa timu za Mbeya ambazo zinakwenda kushindana katika msimu ujao wa ligi kuu.

Timu ya Kyela Combine ikiwa katika furaha ya kufurahia ushindi wa nafasi ya kwanza katika mashindano ya Mbeya Pre season Samia Cup yaliyofanyika hapa wilayani Kyela.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Kyela, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Ismail Mlawa amemwomba Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuipa nafasi wilaya ya Kyela ili mashindano haya yafanyike tena katika wilaya hii ifikapo mwakani.

Nae Afisa Michezo wa Mkoa ndugu Mfugale amesema mashindano ya Mbeya Pre season Samia Cup, yalianzishwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuanzia tarehe 04/08/2022 hadi tarehe 10/08/2022 yakiwa na lengo la kuziandaa timu zote za Mkoa wa Mbeya ambazo zinaenda kushindana katika ligi kuu ya Tanzania, lakini pia kuzipa uzoefu timu ndogo na kuweza kuibua vipaji kwa wachezaji chipukizi.

Katika mashindano ya Mbeya Pre season Samia cup, timu ya Kyela Combine imeibuka mshindi wa Kwanza baada ya kuicharaza timu ya Ihefu Fc kwa goli 1. Hata hivyo timu ya Ihefu fc ilishika nafasi ya 2 ikifuatiwa na timu ya Rungwe Dc.

Mwisho.


Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa