Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera ameziagiza halmashauri zote mkoani hapa kutoa elimu kwa madiwani kuhusiana na mfumo mpya wa ukusanyaji mapato (Tausi) ili kudhibiti upotevu wa mapato wa halmashauri.
Amesema kuwa elimu hiyo itasaidia madiwani kuona umuhimu wa raha ya kukusanya mapato na kuyatumia ikiwa ni pamoja na kuthibiti upotevu wa fedha.
Mhe. Homera amesema hayo tarehe 12/06/2023, katika kikao cha baraza maalum la kupitia hoja za mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali wilayani Kyela, mkutano uliohusisha madiwani, wakuu wa idara na watumishi wa halmashauri pamoja na kamati ya ulinzi na usalama.
“Huu mfumo wa tausi umeletwa kwenye halmashauri zote za mkoa wa Mbeya, sasa Ofisa mapato na uongozi wa halmashauri tengenezeni semina maalum kwa madiwani hata ya siku moja ili kuwaelimisha waheshimiwa madiwani mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato” amesema .
Hata hivyo Mhe. Homera ameeleza kuwa halmashauri zote za mkoa wa mbeya zinatakiwa kuelimisha madiwani kuhusu mfumo huo wa ukusanyaji mapato wa Tausi wajue faida zake na umuhimu wake na namna ya kushirikiana na wakuu wa idara katika ukusanyaji mapato.
Aidha Homera alizungumzia suala la ukusanyaji mapato kwa wilaya ya Kyela imefanya vizuri kwani ilitakiwa kukusanya Zaidi ya Bil.4. mpaka Juni 9, 2023 mmeweza kukusanya Zaidi ya Bil 4 ambayo ni sawa na asilimia 99.72.
“Ndugu zangu wana Kyela pia naomba muache tabia ya kuiua Kyela kimapato naomba ziishe waheshimiwa madiwani kuna wengine hawaitakii mema Kyela kabisa , tusiwadanganye wananchi, si mmeona ufuta kule Songwe wameuza 3700 wakati uuzaji holela ulikuwa shilingi 500 tuache kudanganya na serikali imeshatoa maelekezo kwa mazao ambayo yapo kwenye stakabadhi ghalani kupitia ushirika, likiwemo zao la kokoa ambalo ndilo chanjo kikuu cha mapato wilayani Kyela “amesema .
Diwani viti maalum wilayani Kyela , Tumaini Mwakatika amesema chama cha mapinduzi ni tanuri ambalo linapika vizuri viongozi ambao wanafanya kazi vizuri kwa weledi mkubwa uliotukuka .
“Wewe mkuu wetu wa mkoa umepikwa vizuri tuna taarifa zako hata huko ulikotoka kuwa ulikuwa kiongozi wa mfano hivyo tunakishukuru chama cha mapinduzi kwa jitihada kubwa za kuwandaa viongozi wake kwa umakini mkubwa.
Awari Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa alipata fulsa ya kutembelea bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kiwira Coal Mine, pamoja na kufanya mkutano wa hadhara ili kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Busale kijiji cha Lema.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa