Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase ameshiriki katika zoezi la usafi wa mazingira, katika soko la Lubele kata ya Ikimba, haya yanafanyika ikiwa katika kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania yatakayofanyika 26.04.2024.
Katika zoezi hilo, Mhe.Manase ameendelea kuwasisitiza wananchi kuendelea kuudumisha Muungano na Amani ili tuendelee kuishi kwa usalama na utulivu katika Nchi yetu.
Pamoja na hayo Mhe. Manase ametoa kiasi cha Tsh. 100,000/= kwa wafanya usafi wa soko hilo kwa lengo la kununua Vifaa mbalimbali vitakavyo warahisishia katika ufanyaji wa usafi katika soko hilo.
Mwisho Mkuu wa wilaya ya Kyela amewaahidi Wananchi wa Kata ya Ikimba, kuweka kifusi katika soko hilo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa