• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu Wa Wilaya Ya Kyela Aendelea Kutatua Kero Za Wanachi

Imewekwa Kwenye: July 5th, 2024

Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase ameendelea na ziara yakusikiliza na kutatua kero za wananchi Wilayani Kyela ambapo tarehe 04.07.2024, ametembelea kata ya Lusungo kijiji cha Lukama, kwa lengo lakusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Mhe. Josephine Manase amefanikiwa kutatua kero mbalimbali katika kijiji cha Lukama ikiwemo kero ya upatikanaji wa umeme pamoja na ukosefu wa Mtendaji wa kijiji, ambapo hapo awali hapakuwa na Mtendaji katika kijiji hicho.

Kuhusu suala la umeme, Mratibu wa  "REA" wilaya ya Kyela Ndugu. Jairo Simion Sichura amesema kuwa kijiji cha Lukama kata Lusungo kipo katika mpango wa kuwekewa umeme, na wapo katika hatua ya kumtafuta mkandarasi wa kafanya shughuli hiyo, mara atakapo patikana atatambulishwa katika kijiji na ataanza kazi ya kuwawekea umeme wanakijiji wa Lukama.

Aidha suala la kukosekana kwa mtendaji wa kijiji katika kijiji hicho Mhe. Josephine Manase Mkuu wa wilaya ya Kyela alimtaka Afisa Utumishi wilaya atolee ufafanuzi jambo hilo,  ambapo Ndugu. Michael Celestine Tolage amesema; suala hilo litakamilika baada ya wiki 2, Mtendajibwa kijiji atakuwa amepatikana.

Vilevile kuhusu suala la Elimu, ambapo wanakijiji wa Lukama walitoa malalamiko kuhusu uhaba wa walimu, ambapo Kaimu Afisa Elimu msingi Ndugu, Kanzale Mwangungulu alilitolea ufafanuzi kwa kusema, kuwa pindi Serikali ikitoa ajira za Walimu basi shule ya msingi Lukama itapewa kipaumbele cha kuletewa walimu.

Hata hivyo katika kutilia Mkazo Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amewaambia Wananchi wa Kata ya Lusungo kwa wale wote wenye watoto wao ambao wamesomea kada ya Ualimu wajitolee kwa Muda, katika shule hiyo mpaka pale serikali itakapo toa ajira za walimu.

Akijibu swali la mwanakijiji kuhusu kukithiri kwa mimba za utotoni katika kijiji hicho Mhe. Josephine Manase amesema Ni kosa kubwa kwa mtu kumpa mimba mwanafunzi, aidha Mhe. Manase ameendelea kutoa onyo kali kwa mtu yeyote atakae patikana na hatia hiyo, hatua kali za kisheria zitachuliwa, Hivyo amewataka wananchi hao kushirikiana ili kupiga vita mimba za utotoni.

Pamoja na hayo, Mhe. Mkuu wa wilaya amewataka wananchi waliopata maji majumbani kwao kuyalipia maji hayo, ili kuiwezesha wizara husika kuwafikia watu wengi katika kusambaza huduma ya maji, pia kurekebisha miundo mbinu ya maji pale inapohitajika.

Pamoja nakusikiliza kero za wananchi wa kata ya Lusungo Mhe. Josephine Manase ameendelea kuhamasisha wananchi kuendelea kuilinda na kuitunza amani tuliyonayo Watanzania kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa