• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu Wa Wilaya Ya Kyela Akabidhi Pikipiki 11 Kwa Vikundi 2 Vya Bodaboda Kyela

Imewekwa Kwenye: December 15th, 2021

Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Ismail Mlawa, akizindua moja ya pikipiki ikiwa ni ishara ya kuwakabidhi rasmi,pikipiki 11 kwa vikundi 2 vya Bodaboda.

Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Ismail Mlawa, amekabidhi pikipiki 11 zilizonunuliwa kwa fedha za mikopo inayokana na 10% ya mapato ya ndani kwa vikundi 2 vya bodaboda hapa wilayani kyela, pikipiki hizo zimekabidhiwa siku ya jumatatu tarehe 13/12/2021 katika viwanja vya Halmashauri ya wilaya ya Kyela.

Akikabidhi pikipiki hizo Mheshimiwa Ismail Mlawa amesema;

Anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa uwezo wake mkubwa wa kusimamia Ilani ya Chama Tawala, Ilani inayozitaka Halmashauri zote kutenga 10% ya mapato ya ndani ili kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Na kwa kupitia mapato hayo leo hii halmashauri yetu imeweza kutoa pikipiki 11 kwa vikundi 2 vya vijana.

Kikundi cha Tujijenge kutoka Kyela na kikundi cha Tujitume kutoka Ipinda, wakiwa na furaha kubwa ya kupata mkopo wao na kununua Bodaboda.

Amesema, “Mheshimiwa  Rais aliposema kazi iendelee, alimaananisha kwani kuendelea kwenyewe ndio huku sasa”.

Pamoja na hayo aliwaasa wanavikundi hao kwenda kuzitumia pikipiki hizo katika kazi ambazo zitawasaidia kupata kipato chao kwa njia halali, kinyume na hapo sheria itachukua mkondo wake.

Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa katule G. Kingamkono alitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Mkuu wa wilaya, Mheshimiwa Mbunge, Mkurungenzi mtendaji pamoja na Afisa maendeleo ya jamii wa wilaya kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, hadi kufanikiwa kutoa mikopo yenye tija kama hii.

Pia aliwaasa wanufaika wa mkopo (bodaboda) kuwa waumini wa kulinda mapato ya serikali yasitoroshwe, kwani mikopo hii inapatikana kwa kupitia fedha za makusanyo ya mapato ya ndani. Pamoja na hayo Mheshimiwa Mwenyekiti, aliwahakikishia wananchi kwamba Halmashauri ya wilaya imejipanga katika kutoa mikopo yenye tija kwa kila robo ya mwaka, hivyo ni kazi ya vikundi kujipanga na kupata mikopo hiyo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Ndugu Ezekiel Magehema amesema, anaishukuru serikali kwa kutenga 10% ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa makundi maalum, na halmashauri yetu inayatekeleza hayo. Kwani kwa kipindi hiki halmashauri imetoa shilingi 150,000,000/=, pesa zilizotolewa kwa kufuata taratibu zote za vikao vya kisheria kwa ajili ya mikopo kwa makundi ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Afisa Maendeleo ya jamii wa wilaya ya Kyela, Ndugu Victor Kabuje akijaribu pikipiki 1 kati ya 11, zilizotolewa kwa mkopo wa vijana Kyela. 

Mwisho ndugu Mbwana Limposo kiongozi wa moja kati ya wanavikundi hao, alitoa shukrani zake za dhati kwa viongozi na serikali na kusema, wanashukuru kwa kupata pikipiki hizi kwani kwa sasa wameepukana na pikpiki za malengo.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • BIDHAA FEKI ZILIZOINGIA KWA NJIA HARAMU ZATEKETEZWA KWA MOTO

    July 01, 2025
  • KYELA YAFANIKISHA UNUNUZI WA GARI JIPYA AINA YA TOYOTA HILUX KUPITIA MAPATO YA NDANI KWA TSH. MILLIONI 149.1

    June 30, 2025
  • KYELA YAFANIKISHA UNUNUZI WA GARI JIPYA AINA YA TOYOTA HILUX KUPITIA MAPATO YA NDANI KWA TSH. MILLIONI 149.1

    June 30, 2025
  • KYELA YAFANIKISHA UNUNUZI WA GARI JIPYA AINA YA TOYOTA HILUX KUPITIA MAPATO YA NDANI KWA TSH. MILLIONI 149.1

    June 30, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa