Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe.Ismail Mlawa akimkabidhi baiskeli mwanafunzi Johnson Kilale, wa shule ya sekondari Kyela Day, ambae ni mlemavu wa miguu.
Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Ismail Mlawa amemkabidhi baiskeli, Mwanafunzi Johnson Benson Kilale anaesoma shule ya sekondari Kyela Day, tukio lililofanyika tarehe 28/02/2022.
Aidha Mheshiniwa Mkuu wa wilaya amesema baiskeli hiyo imetolewa na Maafisa kutoka Ikulu ambao walifika wilayani Kyela kwa ajiri ya ukaguzi wa mradi namba 5441 TCRP wa madarasa, Na walipofika katika shule katika shule ya sekondari Kyela Day, walikutana na mwanafunzi Johnson ambae ni mlemavu wa miguu, na kisha kufikisha taarifa hiyo kwa Mhe. Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania na kuagiza kuwa Mwanafunzi huyo atimiziwe mahitaji yake.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa