• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu Wa Wilaya Ya Kyela Azindua Mabweni 2 Bwalo 1 La Chakula Katika Shule Ya Sekondari Kafundo

Imewekwa Kwenye: July 30th, 2022

Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Ismail Mlawa Akizindua Mabweni 2 na bwalo 1 katika shule ya sekondari Kafundo iliyopo kata ya Ipinda wilayani Kyela.

Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mheshimiwa Ismail Mlawa, amezindua mabweni 2 pamoja na bwalo 1 la chakula kwa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera, katika shule ya sekondari Kafundo tarehe 29/07/2022.

Akizindua mabweni hayo 2 pamoja na bwalo 1 la chakula, Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ametoa pongezi zake za dhati kwa wadau wa maendeleo "COCOA FOR SCHOOLS" pamoja na wananchi ambao wameshirikiana kwa pamoja katika kujenga mabweni hayo pamoja na bwalo la chakula. Amesema ujenzi wa mabweni ni msaada mkubwa hasa kwa wanafunzi wa kike, wale wanaotoka mbali na eneo la shule.

Picha ya Mabweni yaliyozinduliwa katika shule ya sekondari Kafundo

Aidha Mheshimiwa mkuu wa wilaya amewataka wanafunzi kukazana kusoma kwa bidii na kuongeza ufaulu kwani lengo la wilaya ni kuwa miongoni mwa wilaya 10 bora katika ufaulu Kitaifa.

Amesema, ili kufikia ufaulu huo wazazi hawana budi kutoa chakula kwa watoto wao wawapo shuleni ili wanafunzi wapate nguvu za kusoma. Hata hivyo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii masomo ya sayansi ili nchi yetu iwe na wanasayansi wengi kwa maendeleo ya nchi.

Akitoa taarifa yake kwa Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Kyela, Mkuu wa shule ya sekondari Kafundo Jenny A. Nombo amesema, pamoja na msaada wa wadau wa maendeleo, Pia anapenda kutoa shukrani za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi 25,000,000/= ambazo zimesaidia ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa kwa ajili ya kuanzisha tahasusi za Sayansi katika kidato cha tano na sita.

Sambamba na uzinduzi wa mabweni hayo Mheshimuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela alipata fulsa ya uzinduzi wa vyumba 13 vya madarasa katika shule ya msingi Nkuyu iliyopo kata ya Nkuyu hapa wilayani Kyela. Madarasa yaliyojengwa na wadau hao wa maendeleo pamoja na nguvu za wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa maendeleo yaani "COCOA FOR SCHOOLS" Mr. Fons amesema lengo la kufadhiri ujenzi huu ni pamoja na kutaka kuona kila mwalimu anakuwa na darasa lake la kufundisha lakini pia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi. Na hata hivyo kwa sasa wanampango wa kujenga madrasa 141 katika wilaya ya Kyela na wilaya ya Rungwe.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya aliendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujitokeza ili kuhesabiwa katika siku ya Sensa ya watu na makazi itakayofanyika tarehe 23/08/2022.

Bwalo la chakula katika shule ya sekondari Kafundo.

Mwisho.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MILIONI 570 ZATOLEWA KWA VIKUNDI VYA VIJANA, WANAWAKE PAMOJA NA WATU WENYE ULEMAVU

    January 07, 2026
  • MKURUGENZI MTENDAJI KYELA ADV. FLORAH A. LUHALA AWATAKA WATUMISHI WAPYA 50 KULINDA NIDHAMU YA KAZI NA KUHUDUMIA WANANCHI

    December 05, 2025
  • THOBIAS JOSEPH MWAMKONDA APITA KWA KISHINDO KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA

    December 02, 2025
  • DC KYELA AONGOZA KIKAO KAZI NA WATENDAJI WA KATA, WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI

    November 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa