• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono Ahamasisha Maendeleo Nduka

Imewekwa Kwenye: November 11th, 2023


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono ametembelea kitongoji cha Nduka kata ya Ngana ili kusikiliza changamoto mbalimbali wanazopitia wakazi wa Kitongoji cha Nduka.

Akizungumza  katika mkutano wa hadhara tarehe 10/11/2023 katika Kitongoji cha Nduka, Mhe. Katule Kingamkono, Amempongeza Mhe. diwani wa kata ya Ngana Mhe. Kajela kwa kukipigania kitongoji cha Nduka, kwani wananchi hao wanapitia changamoto kubwa sana ikiwemo kutokuwepo kwa hospital pamoja na miundo mizuri ya barabara.

Aidha Mhe. Katule Kingamkono amewapongeza wazazi wa kitongoji cha Nduka, kwakuwa na muamko wa Elimu kwa watoto wao, Pia kutambua Umuhimu wa Elimu kwa watoto.

Mhe. Katule Kingamkono ameahidi kuwa bega kwa bega na wananchi wa kitongoji cha Nduka na kuhakikisha na uongozi wa wilaya ili zahanati ijengwe katika kitongoji hicho, kilicho mbali na huduma za afya.

Wananchi wa Nduka katika harakati za kuanza ujenzi wa mradi wa zahanati, wamefyatua tofali elfu 8, Pamoja na kuchanga kiasi cha pesa Tsh Laki 3.

Pamoja na hayo katika harakati za kuunga mkono juhudi za upatikanaji wa zahanati ili kuwakomboa kina mama wajawazito na watoto Mhe. Katule Kingamkono, amechangia kiasi cha shilingi laki 5 na kuahidi kutoa shilingi laki 5 nyingine mara baada ya kupatikana fundi ili ujenzi uanze mara moja.

Vilevile Mhe. Katule, amewataka wananchi katika kitongoji cha Nduka kutokuwa wanyonge kutokana na changamoto zinazowakabili bali kuwa na mshikamano na umoja ili kufikia malengo ya maendeleo,  katika kitongoji hicho.

Pamoja na hayo, Mhe. Katule Kingamkono amewataka Wananduka kuongeza juhudi na maarifa kwa kuanzisha vitega uchumi mbalimbali ili kujikomboa na umasikini katika kitongoji cha Nduka.

Akiunga mkono Juhudi zakujikomboa na umasikini katika kitongoji cha Nduka, Mhe. Katule Kingamkono ameahidi kuwaletea vifaranga vya kuku 20 ili kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku pamoja na kuwaletea miche 500 ya miti ya michikichi.

Wananchi wa Kitongoji cha Nduka wamefurahi na wamemshukuru Mhe. Katule Kingamkono kwa kuwatembelea na kuguswa na changamoto wanazopitia katika kitongoji hicho kwani ni viongozi wachache wenye moyo huo.

Mhe. Katule Kingamkono amehitimisha mkutano huo kwa kuwaomba wazazi wa kitongoji hicho kuwaunga mkono watoto wao katika suala la elimu, kwani elimu ndio msingi bora wa maisha ya mwanadamu.

Mwisho.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • DED KYELA AFANYA KIKAO NA WATENDAJI KATA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA UTENDAJI KAZI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

    April 10, 2025
  • DC KYELA AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KUANZIA JULAI HADI DESEMBA 2024

    March 29, 2025
  • KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAPONGEZA USIMAMIZI MZURI WA MRADI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA

    March 20, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa