• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Serikali Yagawa Miche Zaidi Ya Elfu 30 Ya Chikichi Bure Kwa Wakulima Kyela

Imewekwa Kwenye: February 20th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera(kulia), akimkabidhi mche wa mchikichi mmoja wa wakulima wa chikichiki Kyela ,ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ugawaji wa miche hiyo bure kwa wakulima.

Serikali kwa kushirikiana taasisi ya utafiti wa mbegu (TARI-Uyole), imegawa  bure miche ya chikichi zaidi ya elfu 30 kwa wakulima, zoezi lilifanyika tarehe 19/02/2022 katika kitalu cha michikichi hiyo kilichopo katika halmaahauri ya wilaya ya Kyela.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa miche hiyo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera amesema,

Anamshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulisimamia na kuhasisha zao hili la michikichi kuzalishwa Tanzania, kwani zao hili litasaidia kuondoa upungufu mkubwa wa mafuta katika nchi yetu.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera akiwa katika moja ya kitalu cha michikichi katika eneo la Halmashauri ya wilaya ya Kyela.

Aliongeza kwa kuwapongeza watalaam wa TARI Uyole pamoja na wataalam kutoka halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuzalisha miche ya zao la mchikichi.

"Miche zaidi ya elfu 30 itagawiwa kwa wakulima kwa mara ya kwanza hapa wilayani Kyela" alisema. Pia alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri, afanye utafiti wa ugonjwa wa kakao kwa kutumia fedha shilingi 5 inayopatikana katika makato ya shilingi ishirini inayokatwa kwa kila kilo 1 ya kakao katika mauzo yake.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Kenneth Nzilano akipanda mche wa chikichi ikiwa ni ishara ya muendelezo wa uzalishaji na upandaji wa zao la michikichi Wilayani Kyela.

Nae Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono
Alisema, anayofuraha kubwa leo kuona Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa akizindua zoezi hili la kugawa michikichi bure kwa wakulima wilayani Kyela, Pia alisema Kyela tumejipanga kila agizo linalotolewa na viongozi, tunalitekeleza, aliwaomba wataalam wa TARI Uyole kuendelea kuzalisha Mbegu bora za mazao mbalimbali ili wakulima wetu wapate kufaidika zaidi.

Doris Mwasonga(mwananchi), alitoa shukrani kwa Viongozi wa serikali kwa kuwagawia michikichi bure.

Pamoja na zoezi hilo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliweza kutembelea kituo cha "One Stop Border Post", Aliweza kukagua ujenzi wa taa za barabarani katika barabara ya Kikusya matema ambapo taa zaidi ya 60 zitawekwa katika mji wa Ipinda na baadae Kyela mjini.

Aidha Mheshimiwa Juma Homera alitembelea katika kijiji cha Masebe kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja lililowasumbua wananchi kuanzia miaka ya 1972, ambapo wananchi wa kijiji hicho wameishukuru Serikali kwa kuwakumbuka, Pia walimshukuru Mbunge wa Jimbo la Kyela Mheshimiwa Ally J. Kinanasi kwa kuwapigania wanakijiji hao nakuondoa kero hiyo ya miaka mingi kwa wananchi hao.

Pia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa alitembelea ujenzi wa mradi wa barabara za rami zenye urefu wa km 2.2 hapa mjini Kyela, Na alifanikiwa kufika katika Bandari ya Itungi ili kufahamu kitu gani kinachosababisha meli ya abiria kutofanya safari zake.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA YA KYELA APOKEA BOTI YA DORIA KWA AJILI YA ZIWA NYASA

    August 23, 2025
  • MKUU WA WILAYA KYELA AONGOZA TATHMINI YA MICHEZO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA.

    August 16, 2025
  • DC MANASE AENDELEA NA ZIARA YA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHII

    August 13, 2025
  • DC MANASE ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA NISHATI SAFI

    August 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa