Haya yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Claudia U. Kitta alipokuwa akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF), hapa wilayani Kyela tarehe 27/03/2019.
Akitoa ufafanuzi huo amesema; watalaam kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kyela hupita kutoa elimu ya matumizi bora ya fedha wanazozipata walengwa kwa kila dirisha la malipo linapofunguliwa. Hivyo walengwa wengi wanapewa elimu juu ya matumizi ya pesa ambayo inatolewa ili kuwasaidia wananchi wote waishio katika mazingara magumu.
Aidha alisema, mfuko huu umesaidia sana katika kuongeza nguvu kazi hapa wilayani Kyela, kwani mfuko huu umewagusa hata wananchi ambao ni waathirika wa VVU, ambao walikuwa hawana uwezo wowote wa kujipatia chakula, na hivyo kufanya afya zao kuathirika zaidi.
Pamoja na hayo walengwa wengi ambao ni waathirika wa VVU na wale wazima, kwa pamoja wameishukuru serikali ya awamu ya tano, kwa kuwasaidia kupata hiki kidogo ambacho kimewasaidia kupata chakula, na kuwa na afya njema inayowasaidia wao kufanya shughuli ndogondogo za kimaendeleo na kuinua kipato chao.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Kyela, amekuwa akifanya ziara za kutembelea walengwa wote wanaonufaika na mfuko huu. Hata Kama kuna mazuri mengi ambayo yamekuwa yakifanywa na mfuko huu, ila kwa upande wake, amegundua changamoto ya watendaji kuchelewa kufika katika eneo la malipo na kufanya malipo kwa walengwa.
Amesema, tatizo hili linaweza kusababisha usalama mdogo wa fedha za walengwa, Hivyo kwa kupitia changamoto hii Mkuu wa wilaya ya Kyela, amewataka watendaji na wahusika wote wanashughulika na malipo haya kuwahi kufika eneo la malipo ili kuondoa changamoto ya usalama kwa wapokeaji wa fedha hizo.
Aidha alitoa shukrani zake za dhati kwa serikali ya awamu ya tano, kwa kusaidia wananchi wake kupitia mfuko huu wa TASAF, kwani kuna baadhi ya wanufaika wameweza hata kuanzisha vikundi vya kukopeshana.
Kikundi cha Mwamko, kinachopatikana kijiji cha Kilombero kata ya Mababu hapa wilayani Kyela, ni moja kati ya vikundi vilivyofanikiwa kuchanga fedha hadi kufikia kiwango cha zaidi ya shilingi 1,500,000/= wakiwa na wanachama 20 chini ya mwenyekiti wao Essah Ijande.
Wanasema; wametumia elimu iliyokuwa ikitolewa na watalaam kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kyela, elimu iliyokuwa ikisisitiza swala la walengwa kuunda vikundi na kusaidiana ili kukuza mitaji yao.
Wanakikundi hawa kila walipopata fedha katika dirisha la malipo, waliweza kuchangia kiasi cha shilingi 1000/= kwa kila mjumbe, hivyo pesa hiyo iliwasaidia kununua vifaranga 100 vya kuku na kugawana, ambapo hadi sasa kila mjumbe anakuku wasiopungua 15.
Aidha fedha zilizobaki zimewasaidia kuanzisha shughuli za kilimo kwa kukodi mashamba mawili, ambayo wamepanda mpunga, wanaotegemea kuvuna gunia zaidi ya 18.
Kikundi hiki kimekuwa na malengo mengi na makubwa kwa baadae, mfano; wamepanga kununua mashine ya kusaga na kukoboa, kununua shamba lao la kudumu, kufungua akaunti benki pamoja na kupata usafiri wa baiskeli ya kikundi.
Mwisho pongezi nyingi zilitolewa na wanufaika kwa serikali yao inayowajali, kwani imeweza kuwaondoa katika umaskini uliyokuwa umekisili miongoni mwao, pia imepunguza maradhi kama utapyamulo katika jamii zao.
Mmoja wa wanakikundi cha Mwamko akiwa na baadhi ya kuku wake
Baadhi ya wajumbe wa kikundi cha Mwamko wakiwa katika picha ya pamoja.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa