• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Tuilinde Miradi Inayotekelezwa Na Serikali-Albert Chalamila

Imewekwa Kwenye: February 25th, 2021

Haya yamezungumzwa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kyela katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo, ziara iliyofanyika katika kata za Ipinda, Matema na Mababu hapa wilayani Kyela tarehe 24.02.2021.

Akizungumza na wananchi katika mradi wa maji uliopo kata ya Mababu wilayani Kyela Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema ni vizuri wananchi wakawa ni walinzi na kuipa thamani miradi hii yote inayotekelezwa na serikali yao, ikiwa ni pamoja na kuitunza miundo mbinu yote ya miradi ya maji ambayo inatekelezwa katika wilaya ya Kyela.

Pia Mkuu wa mkoa amewataka wananchi kuchangia miradi inayoletwa na serikali ili kuifanya miradi hiyo kutekelezwa kwa haraka, aliongeza kwa kusema michango si lazima iwe fedha, bali hata kutoa baadhi ya maeneo ya kijiji ili kurusu miradi kutekelezeka .

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji, meneja wa maji Kyela Eng. Tanu Deule amesema; miradi hii ya maji hadi kukamilika kwake itatumia kiasi cha shilingi 29,547,000/= kwa mradi wa maji wa Matema katika vitongoji vya Ibungu na Lyulilo pia shilingi 344,918,750 kwa mradi wa maji wa Mababu. Na kwa mradi wa maji wa Mababu hadi sasa kiasi  zaidi ya shilingi 90,000,000/= zimeshatumika. 

 

Aidha Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Claudia U. Kitta alitoa pongezi kwa wananchi wa Lyulilo kwa kupata maji safi na salama kwani  ni kwa takribani miaka 10, wananchi hao hawajapata maji ya bomba. Pia alitoa shukrani, pongezi kwa  kazi kubwa inayofanywa na serikali, Kwani Kyela imependelewa sana kwa kuletewa miradi mingi ya maendeleo. Aidha aliwasii wananchi kuilinda na kuithamini miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa na serikali yetu.

Mwisho Mhe. Mkuu wa mkoa alipata nafasi ya kutembelea ujenzi wa mabweni matatu (3 ) na bwalo moja (1) la chakula , yanayojengwa katika shule ya sekondari Kafundo iliyopo kata ya Ipinda hapa wilayani Kyela, Huku akiwahimiza wazazi kutoa huduma ya chakula kwa wanafunzi wao shuleni, ili kuwafanya kuwa na afya njema na kuwa na ufikiri mzuri katika masomo yao wawapo darasani.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya (kulia kavaa kofia) akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu. Ezekiel Magehema (kushoto), akiwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule Kingamkono(nyuma ya mkurugenzi) pamoja na viongozi wengine wakitembelea ujenzi wa mabweni katika shule ya sekondari Kafundo iliyopo kata ya Ipinda hapa wilayani Kyela.

IMETOLEWA NA;

OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO

KYELA.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa