• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wanafunzi Wote Wa Shule Ya Msingi Nduka Wanunuliwa Sare Za Shule Na Viatu

Imewekwa Kwenye: February 6th, 2022

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono akikabidhi msaada wa sare za shule na viatu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Nduka.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Nduka, iliyopo kata ya Ngana wilayani Kyela wamenunuliwa na kugawiwa sare za shule pamoja na viatu, ikiwa ni ombi la wanafunzi hao kwa Mheshimiwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela wakati alipofanya ziara katika shule hiyo takribani mwezi 1 uliopita. Sare na viatu hivyo vimegawiwa tarehe 05/02/2022 zoezi lililofanyika katika kata ya Ngana.

Akizungumza na wananchi hao Mheshimiwa Katule alisema, anapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia na hata kufanikiwa kuwanunulia sale na viatu vya shule wanafunzi hao, na anafanya hivi ili kukisaidia kizazi cha Nduka kufanikiwa katika elimu."

Wawakiliashi wa wanafunzi wa shule ya msingi Nduka wakiwa wamepoke sare za shule na viatu.

"Msaada huu si wangu peke yangu bali ni msaada kutoka kwangu na wadau wengine wa maendeleo ikiwa ni pamoja na  mawazo mazuri ya viongozi wote wa wilaya ya Kyela, ila kwa upande wangu nitakuwa pamoja na wanaNduka kwa miaka yangu yote ya uongozi wangu hata nikiwa nje ya uongozi" alisema.

Pia Mheshimiwa Mwenyekiti alimuagiza mtendaji wa kata kuhakikisha wanakijiji cha Nduka wanapata miche ya michikichi ambayo inagawiwa bure na Halmashauri kwa wakulima.

Akiongea kwa niaba ya wananchi diwani wa kata hiyo Mheshimiwa Kajala alisema, Tunashukuru Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kutimaza ahadi zako, uliahidi kuwaletea wanafunzi daftari na umeleta, uliahidi kuleta sare za wanafunzi pamoja na viatu na umeleta, usafiri kwa walimu pamoja na umeme haya yote umeyafanya na yanatekelezwa.Mwisho Mheshimiwa diwani aliwataka wananchi wa Nduka kutekeleza ushauri alioutoa Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela, ushauri uliowataka wanakijiji cha Nduka kuishi kwa pamoja ili kuanza kupata huduma za msingi  kwa pamoja.

Nae kaka mkuu wa shule Brain Benson alisema anashukuru kwa niaba ya wanafunzi wenzake, kwa kupata sare za shule na kwa niaba aliahidi kuwa watasoma kwa bidii.

Wanafunzi wa shule ya msingi Nduka wakisubiri kukabidhiwa sare na viatu vya shule kutoka kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wialaya ya Kyela.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa