• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wilaya Ya Kyela Yafanya Maadhimisho Ya Kilele Cha Siku Ya Mazingira Duniani

Imewekwa Kwenye: June 6th, 2023

Maadhimisho ya siku ya mazingira yafanyika wilayani Kyela tarehe 05/06/2923 kwa upandaji wa miti katika shule ya msingi Sama.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi wa NEMC kanda za juu kusini, wakuu wa idara na vitengo mbalimbali, wadau wa mazingira pamoja na wananchi.

Akizungumza wakati akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kyela, Afisa tarafa ya Unyakyusa ndugu Kheri L. William amesema;

Lengo kuu la Maadhimisho ya siku ya Mazingira mwaka huu ni kufanya tathmini ya Mazingira, kubaini changamoto zinazoikabili Sekta ya Mazingira na kutoa mwelekeo wa kupambambana na changamoto hizo ili kuwa na Mazingira bora na endelevu, tukiongozwa na kauli mbiu ya mwaka ya mwaka huu Kitaifa ″Pinga uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki”

Aidha amesema Halmashauri ya Kyela imepanda jumla ya miti 70,700, katika maeneo mbalimbali kama shuleni, vijiji, Zahanati na katika vituo vya afya. Pia usafi umefanyika kwenye maeneo ya mifereji, masoko na fuke ya Ziwa Nyasa.

Shughuli hizo ziliambatana na uhamasishaji wa wananchi katika masuala ya uhifadhi na usafishaji wa mazingira yanayowazunguka.

Pamoja na hayo Ndugu Kher L. William amebainisha athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kama ilivyo kwa nchi nzima na dunia nzima ambazo asilimia kubwa zimetokana na shughuli za kibinadamu.

Amesema  Athari hizo huambatana na milipuko ya magonjwa ya mara kwa mara kwa binadamu, mifugo na kilimo, kuharibika kwa mifumo ya ikologia inayotokana na kuongezeka kwa hali ya joto, kuongozeka kwa maji ya Ziwa/bahari.

Awali Kaimu meneja kanda za juu kusini "NEMC", ndugu Milton Patrick Mponda amesema, Serikali imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki, baada ya kufanya tafiti na kujiridhisha kwamba, kuna hasara nyingi za matumizi ya mifuko hiyo kuliko faida zake.

Hivyo hairuhusiwi kutumia bidha hizi mahali popote, iwe dukani, sokoni au sehemu yoyote ya mikusanyiko ili kulinda mazingira.

Pamoja na hayo amesema nchi yetu imetunga sheria kali amabazo zinazuia utengenezaji, uingizaji, umiliki, na usambazaji wa bidhaa hizo ikiwa ni kwa lengo la kulinda mazingira na vyanzo vya maji.

Mwisho Wananchi wa Wilaya ya Kyela yatupasa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita za kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya kuhimiza usafi na utunzaji wa mazingira.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa