Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imenunua gari aina ya Toyota Hilux kwa gharama ya TSH. 149,194,457.85 kupitia mapato yake ya ndani, ikiwa ni hatua madhubuti ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.
Kupatikana kwa gari hili kutaongeza ufanisi mkubwa katika kufanikisha ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye kata mbalimbali ndani ya Wilaya ya Kyela. Pia, litarahisisha kazi za uratibu wa shughuli za wataalam wa Idara mbalimbali kama vile kilimo, afya ,elimu,Mipango, utawala, Fedha, n.k. ambao mara kwa mara huhitaji kusafiri kufuatilia utekelezaji wa shughuli mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya kyela
Katika kuonesha dira njema ya uongozi, viongozi wa Halmashauri ya Kyela wameendelea kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato ya ndani, hatua iliyowezesha kufanikisha ununuzi huu muhimu. Mchango wa viongozi hawa hauishii kwenye ukusanyaji wa mapato pekee bali pia unaonekana katika matumizi yenye tija ya fedha za umma kwa manufaa ya wananchi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa