IDARA YA ELIMU MSINGI
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ina jumla ya shule za msingi 105. Kati ya hizo kuna shule za binafsi 2. Shughuli zote za idara zinasimamiwa kupitia vitengo 5 kama ifuatavyo:
2.1 Idadi ya wanafunzi
Idadi ya wanafunzi wa madarasa ya awali ni 6,448 wakiwemo wavulana 3,320 na wasichana 3,078 kwa shule 103 za Serikali na wanafunzi 81 kwa shule binafsi ambapo kati yao wavulana ni 49 na wasichana 32. Kati ya shule 103 za msingi za Serikali, shule moja ni ya mchepuo wa Kiingereza inayoitwa Nyasa English Medium Primary School.
Idadi ya wanafunzi wa darasa la I – VII ni 48789 ambapo kati yao wavulana ni 24596 na wasichana ni 24193 kwa shule za serikali na wanafunzi 375 wa shule binafsi ambapo kati yao wavulana ni 163 na wasichana ni 212.
Aidha, jumla ya wanafunzi wote kuanzia awali hadi darasa la VII ni 55,237 ambapo wavulana ni 27,966 na wasichana ni 27,271 kwa shule za Serikali.
Hali ya walimu wa shule za msingi hadi 30 Desemba, 2020 ni 896 ambapo wanaume ni 446 na wanawake ni 450. Uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi ni 1:62. Hata hivyo Serikali imeajiri walimu 19 katika Halmashauri yetu ambapo wengine wanaendelea kuripoti.
2.2 Watoto wenye mahitaji maalumu
Halmashauri ina shule 2 zenye vitengo vya watoto wenye mahitaji maalum ambavyo ni shule ya msingi Kyela na Mwenge. Vitengo hivi vina jumla ya wanafunzi 68. Pia kuna kitengo cha wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya sekondari Kyela chenye wanafunzi 12. Aidha, Halmashauri ina mpango wa kuanzisha vitengo 2 katika shule za msingi Sama na Matema kwa ajili ya watoto wasioona na wenye matatizo ya akili.
Pia kuna vituo vya elimu ya watu wazima vyenye jumla ya wanafunzi 94 na vituo vya MEMKWA 12 vyenye jumla ya wanafunzi 144.
2.3 Hali ya ufaulu wa wanafunzi wa darasa la VII kuanzia 2015 – 2019
Hali ya ufaulu wa wanafunzi wa darasa la VII imekuwa ikipanda kutoka mwaka 2015 hadi 2019 kama jedwali linavyoonesha hapa chini;
Mwaka |
Waliofanya
|
Waliofaulu
|
% ya Ufaulu
|
waliochaguliwa
|
||||||
wav
|
Was
|
jml
|
wav
|
was
|
jml
|
wav
|
was
|
jml
|
||
2015
|
3299
|
3570
|
6869
|
2115
|
1889
|
4004
|
58.29
|
2115
|
1889
|
4004
|
2016
|
3510
|
3781
|
7291
|
2048
|
2313
|
4361
|
59.82
|
2048
|
2313
|
4361
|
2017
|
3624
|
3714
|
7338
|
2418
|
2210
|
4628
|
63.07
|
2418
|
2210
|
4628
|
2018
|
3422
|
3509
|
6931
|
2654
|
2619
|
5273
|
76.08
|
2654
|
2619
|
5273
|
2019
|
2888
|
3109
|
5997
|
2529
|
2660
|
5189
|
86.51
|
2529
|
2660
|
5189
|
Aidha, kutoka mwaka 2006 hadi mwaka 2019 wanafunzi wote waliofaulu walijiunga na kidato cha kwanza.
2.4 Hali halisi ya miundombinu na samani
Na.
|
Miundombinu
|
Mahitaji
|
Iliyopo
|
Upungufu
|
% ya upungufu
|
1
|
Madarasa
|
1359
|
849
|
510
|
37
|
2
|
Nyumba za walimu
|
1359
|
191
|
1168
|
86
|
3
|
Matundu ya vyoo
|
2358
|
1364
|
994
|
42
|
4
|
Madawati
|
16626
|
17582
|
1338
|
8
|
2.5 Changamoto zinazoikabili idara
Idara ya usafi wa mazingira inatekeleza majukumu yafuatayo:-
CHANGAMOTO.
Idara ya Elimu ya Sekondari ina shule 28 zikiwemo shule 22 za serikali na shule 6 za binafsi. Idara ina jumla wanafunzi 15580 kwa shule za serikali na jumla ya walimu 678.
Idara ya Elimu Sekondari inayo jumla ya watumishi sita wa makao makuu ya Halmashauri ambao ni Afisa Elimu Sekondari, Afisa Elimu vifaa na Takwimu, Afisa elimu Taaluma Sekondari, Mtunza kumbukumbu za ofisi, Dereva na Mhudumu wa Ofisi.
Idara inatekeleza majukumu yafuatayo;
Kusimamia sera na miongozo inayotolewa na Serikali kuhusu elimu ya sekondari ndani ya wilaya.
Kusimamia, kuratibu na kufuatilia shughuli za ujenzi wa miundombinu katika shule za sekondari kama vile nyumba za walimu, madarasa, majengo ya utawala, maabara, makitaba na vyoo.
Kusimamia na kuratibu shughuli zote za ukusanyaji, uchambuzi na kutafsiri takwimu za Idara ya elimu sekondari na kuwasilisha sehemu husika.
Kusimamia na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata taaluma kwa kiwango kilicho bora kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya mwaka 1995 na 20014.
Kusimamia na kuhakikisha nidhamu ya wanafunzi, walimu na watumishi wasio walimu inadumishwa shuleni.
Kuandaa mpango na maksio ya bajeti ya idara ya Elimu ya Elimu Sekondari kila mwaka.
4.1 MIUNDOMBINU
MADARASA
|
VYOO
|
NYUMBA ZA WALIMU
|
||||||
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
Mahitaji
|
Yaliyopo
|
Upungufu
|
417
|
393
|
33
|
607
|
362
|
230
|
622
|
51
|
571
|
Baadhi ya shule zimefika ukomo wa kuongeza madarasa kwa kuwa zimekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi. Ufumbuzi ni kujenga shule mpya katika maeneo ambayo shule zake zimejaa mfano Kyela mjini idadi kubwa ya wanafunzi wanahitimu kila mwaka na kuwapeleka katika kata za pembezoni.
Kwa kuzingatia hilo idara imeandika andiko juu ya ujenzi wa zaidi ya vyumba 87 katika shule zilizopo na ujenzi wa shule mbili(2) mpya unaendelea katika kata za Busale na Njisi. Aidha, Ujenzi katika kata ya Busale unaendelea vizuri wakati kwa kata ya Njisi kasi sio nzuri.
Mpango mwengine ni ujenzi wa shule za Hosteli kwa ajili ya wasichana, kwa kuanzia tulitenga shule ya Nyasa kwa kupeleka wanafunzi waliofaulu vizuri zaidi katika ngazi ya wilaya, tumepeleka wanafunzi kwa miaka 2 lakini kwa mwaka huu tumeshindwa kutokana na kukosekana kwa bweni.
Uhitaji wa huduma hii ni mkubwa kwani wazazi wengi wilayani Kyela wamekuwa wanahangaika kupeleka watoto katika wilaya za jirani kwenye hosteli.
4.2 UFAULU
Ufaulu wa wanafunzi kwa ngazi ya Halmashauri umekuwa ukiongezaka ingawa tukilinganisha na Halmashauri zingine bado tunahitaji kuongeza nguvu zaidi.
Ufaulu Kidato cha Nne
Mwaka 2017
|
Mwaka 2018
|
Mwaka 2019
|
||||||
Waliofanya
|
Waliofaulu
|
Asilimia
|
Waliofanya
|
Waliofaulu
|
Asilimia
|
Waliofanya
|
Waliofaulu
|
Asilimia
|
1956
|
1515
|
77.5
|
2088
|
1647
|
78.9
|
2546
|
2048
|
80.4
|
Ufaulu Kidato cha Sita
Mwaka 2017
|
Mwaka 2018
|
Mwaka 2019
|
||||||
Waliofanya
|
Waliofaulu
|
Asilimia
|
Waliofanya
|
Waliofaulu
|
Asilimia
|
Waliofanya
|
Waliofaulu
|
Asilimia
|
367
|
363
|
98.9
|
198
|
196
|
99.0
|
198
|
198
|
100
|
4.3 MIKAKATI
Ujenzi wa hosteli na kuzitumia
Uchangiaji wa chakula cha mchana ili watoto wapewe muda wa ziada
Makambi kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani
Aidha, mbinu hizi zimeonesha kutoa matunda kwani tuna shule za mfano ambazo zimeonesha matokeo haya.
Matokeo ya mwaka 2019 shule yetu ya Masukila Sekondari imeingia katika Shule kumi bora kitaifa kwa kushika namba ya 5 ikiwa ni shule pekee kwa mkoa wa Mbeya kwa Shule za Serikali
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa