Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo wa Kyela Mhe.Emmanuel K. Bongo ameongoza Mkutano wa Baraza maalumu katika ukumbi wa Mamlaka tarehe 1.10.2025.
Mkutano huo umeambatana na uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji mdogo pamoja na uchaguzi wa kamati za kudumu Kwa mwaka wa fedha 2025/26 Kamati hizo ni Elimu na Afya,Uchumi Ujenzi na Mazingira,Fedha uongozi na mipango, maadili, na kamati ya kudhibiti ukimwi na kifua kikuu.
Mhe.Bongo amewataka wajumbe wa Baraza hilo kuwa waadilifu na kujenga ushirikiano mzuri kwa viongozi waliochaguliwa ili waweze kufanya kazi kwa wepesi utakaoleta maendeleo kwa Wananchi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa