Wah.Madiwani Wilaya ya Kyela Leo tar 2.Dec 2025 wameapishwa rasmi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Zoezi hilo limeambatana na uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo Wah.madiwani walimchgua
Mhe.Thobias Mwamkonda kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kwa mwaka 2025-2030.
Mhe.Mwenyekiti Mteule Thobias Mwamkonda amewashukuru wajumbe kwa kumchagua na ameahidi kuwa mwadilifu na kutoa ushirikiano mzuri kwa viongozi hasa katika masuala ya utekelezaji wa majukumu yenye manufaa kwa Wananchi wa Wilaya ya Kyela.
Pia amesema Baraza limejipanga kufanya kazi kwa juhudi ikiwemo kuwafikia Wananchi ili waweze kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josphine Manase amewapongeza Wah.madiwani kwa kuchaguliwa kuwa wawakilishi wa Wananchi, na amewataka kujenga ushirikiano na viongozi wengine waliopo kwenye kata zao ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinaendana na kasi ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mhe.Manase amewataka Wananchi wilayani Kyela waendelee kuilinda amani iliyopo Nchini, kujiepusha na masuala yoyote yanayosababisha vurugu na kuharibu miundombinu inayonufaisha Wananchi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa