Mbunge wa Jimbo la Kyela Mhe. Baraka Ulimboka Mwamengo amekabidhi hundi ya mfano ya Tsh. 570,400,000/= kwa vikundi 68 vilivyonufaika na mikopo ya 10% inaoyotolewa kwa Wanawake,Vijana ,na watu wenye ulemavu.
Akikabidhi hundi hiyo tarehe 8.1.2026 katika ukumbi wa Sisita Mhe. Baraka Mwamengo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa mikopo ya 10% inaoyotolewa bila riba kwa lengo la kuinua uchumi wa Wananchi.
Mhe.Mbunge amevitaka vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo kutumia pesa hizo kiuhalali kwa kufanya shughuli zilizo rasmi ili waweze kukuza mitaji na kuinua uchumi wa Taifa.
Akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg.Keneth Nzilano amesema Halmashauri inaendelea na jitihada ya ukusanyaji mzuri wa mapato ili iendelee kutoa mikopo itakayowanufaisha Wananchi.
Kwa upande wao wanufaika wa mikopo hiyo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa mikopo itakayoenda kuboresha na kubadilisha maisha kwa kufanya shughuli zitakazowaingizia kipato.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa