IDARA YA MAENDLEO YA JAMII
Shughuli zinazotekelezwa na idara ya maendeleo ya jammi kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.
Kuhamasisha jamii kwa kuamsha ari kushiriki shughuli za maendeleo katika jamii katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kuchangia nguvu zao na kuchangia fedha kwa maendeleo yao.
Kuratibu masuala ya ukatili wa Kijinsia katika Wilaya, ikiwa ni pamoja na kuratibu Mpango wa kuzuia Ukatili kwa wanawake na Watoto MTAKUWWA katika ngazi ya Jamii.
Kuratibu masula ya vikundi katika Wilaya kwa kuvisajili na kusimamia uendeshaji wao na utatuzi wa migogoro inayojitokeza katika vikundi.
Kuratibu Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na Vijana Ili kuwezesha Kiuchumi makundi hayo maalumu katika jamii kwa kutoa mikopo Isiyo na riba Kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na Watu Wenye Ulemavu kwa asilimia 10 ya mapato yanayotengwa na Halmashauri.
Kuratibu Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs), kuhakikisha yanafanya kazi kwa kuzingatia sheria Na. 24/2002 ya uanzishwaji wa mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Kuratibu Mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI katika jamii ili kupunguza maambukizi mapya na kuhakikisha waliopimwa wanadumia dawa za Kufubaza virusi vya UKIMWI hasa ukizingatia maambuzi ni asilimia 9.3 zaidi ya maambukizi ya Kitaifa ambayo ni asiimia 4.7
Kuratibu shughuli za TASAF kiwilaya kwa kuwezesha kaya masikini kuwapatia fedha kaya maskini iliyoko kwenye mpango.
Kuwezesha usajili wa Vizazi na Vifo kwa Watoto Chini ya Miaka 5 na watu wazima.
Kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora katika Jamii ili kuboresha makazi bora katika jamii zetu.
Kusimamia masuala ya vijana katika jamii ili kujitambua na kutambua fursa zilizopo Wilayani na kuzitumia kujiletea maendeleo.
Kuratibu masuala ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF) ili jamii ijiunge na kupata matibabu kwa gharama nafuu.
Kutoa elimu ya Lishe katika jamii ili kupata jamii yenye afya bora inayoweza kuchangia maendeleo katika jamii na elimu hii husisitiza sana lishe bora kwa Watoto wadogo wanaokuwa na hasa chini ya miaka 5
CHANGAMOTO
Uhaba wa wataalam katika Wilaya ambao unapelekea baadhi ya kata kukosa watumishi.
UTATUZI WA CHANGAMOTO
Tunatumia watumishi wa ugani wa idara zingine waliopo ngazi ya Kata kusaidia baadhi ya majukumu ya idara, pia kila mwaka tunaweka kwenye bajeti.
Halmashauri kupitia Idara ya Ardhi na Maliasili infanya kazi zifuatazo:-
Changamoto zinazotukabili katika idara ya Ardhi na Maliasili.
13. KITENGO CHA MANUNUZI
Kwa mujibu wa Muundo wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela (Organisation Structure) na Sheria ya Ununuzi ya Umma Na.7 ya Mwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2013, Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi kina majukumu yake kama ifuatavyo:-
Kusimamia majukumu yote ya ununuzi na Uuzaji kwa njia ya zabuni mali za Halmashauri kwa kufuata sheria na kanuni za manunuzi
Kusaidia kazi zinazofanywa na bodi ya zabuni
Kutekeleza maagizo ya bodi ya zabuni
Kuandaa mpango wa ununuzi wa Halmashauri na kusimamia utekelezaji wake
Kusimamia utunzaji wa ghala na Nyaraka (kumbukumbu ya vitu vilivyomo ghalani
Kukagua na kuandaa mahitaji ya manunuzi ya Idara na Vitengo katika Halmashauri
Kuandaa nyaraka za zabuni
Kuandaa matangazo ya huduma ya zabuni mbalimbali
Kuandaa taarifa ya kila mwezi ya manunuzi ya Idara na Vitengo na kuiwasilisha katika bodi ya zabuni
Kuandaa mikataba iliyoidhinishwa kwa wazabuni
Kutunza na kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za ununuzi na uuzaji wa mali za hamashauri;
Kuandaa na kuhifadhi rejista ya mikataba ya wazabuni wanaoshinda zabuni;
Kuandaa taarifa za kila siku zinazofanyika katika stoo kuwezesha uhakiki wa mali na utunzaji katika stoo.
Kumshauri Mkurugenzi kuhusu manunuzi kwa kufuata kanuni na sheria.
Kushirikiana na Idara zingine katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Kutekeleza maagizo mengineyo kutoka katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa