Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase ameongoza maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani katika Kata ya Bujonde tarehe 28.11.2025.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mhe.Josephine Manase amesema maadhimisho haya yana lengo la kutoa ujumbe na Elimu kwa Wananchi ili kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.
Pia Mhe.Manase amesema anafahamu kuwa kamati za kudhibiti Ukimwi ngazi ya Wilaya kata na Vijiji zinafanya kazi ipasavyo hivyo ametoa wito kwa kamati hizo kuimarisha huduma na kuhakikisha zinawafikia Wananchi ili waweze kukabilina na janga hili.
Mkuu wa Wilaya amewataka watoa huduma za afya kutoa elimu Shuleni pia amewaasa Wazazi kutoa elimu kwa watoto wao juu ya athari ya ugonjwa wa ukimwi ili waweze kutambua na kulinda afya zao
Aidha Mhe. Manase ametoa msisitizo kwa Wananchi kutokua na mtazamo hasi juu ya ugonjwa wa Ukimwi pia amewataka Wananchi kujenga utaratibu wa kupima ili kujua afya zao na kuchukua tahadhari ya kujikinga zaidi.
Kauli mbiu "Shinda vikwazo,imarisha mwitikio tokomeza ukimwi."
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa