IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
Idara ya Mifugo na Uvuvi inatekeleza majukumu yake kwa wafugaji na wavuvi kama inavyoonesha hapa chini:-
Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji katika kata zote za Halmashauri.
Kukagua nyama na usafi wa machinjio mara kwa mara.
Kutibu magonjwa ya mifugo na kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa.
Kutembelea wafugaji mara kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalam.
Kukusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo la Halmashauri.
Kufanya uhamilishaji (Artificial Insemination) na uzalishaji (breeding) wa mifugo kwa jumla.
Kushauri wafugaji umuhimu wa kupunguza mifugo yao kulingana na maeneo/malisho.
Kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa na viumbe waharibifu.
Kuandaa ratiba cha chanjo na mipango ya uchanjaji.
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wakala wa pembejeo muhimu za mifugo.
Kuwa kiungo kati ya vikundi vya wafugaji na watafiti.
Kukagua na kuidhinisha vibali vya usafirishaji wa mifugo.
Kuendeleza uvunaji endelevu wa samaki na viumbe wengine wa baharini, maziwa, mito, mabwawa na malambo
Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu uvuvi bora, utengenezaji na uhifadhi bora wa samaki na mazao ya uvuvi, biashara na masoko ya samaki pamoja na ufugaji wa samaki na viumbe wengine wa majini
Kutoa leseni za uvuvi na kuendesha mafunzo ya taaluma ya uvuvi.
Kusimamia na kutekeleza sheria za uvuvi (kwa mfano kuzuia uvuvi haramu).
Kuratibu shughuli za utafiti wa uvuvi.
Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali ya uvuvi.
Kukagua ubora wa samaki na mazao ya uvuvi na kuweka viwango vya kitaifa
|
CHANGAMOTO/MAHITAJI
|
UTATUZI /SULUHISHO
|
1.
|
Ukosefu wa vitendea kazi kwa maafisa ugani (pikipiki, extension kits, life jackets)
|
Kupatikana kwa vitendea kazi hivi kwa kutenga fedha katika bajeti ya Halmashauri
|
2.
|
Kukithiri kwa uvuvi haramu
|
Kupatikana kwa boti ya doria kuthibiti uvuvi haramu
|
3.
|
Kutokuwepo kwa machinjio ya kisasa ya kuchinjia ng’ombe
|
Ili kuongeza mnyororo wa thamani kunatakiwa kupatikana kwa machinjio ya kisasa kupitia wadau mbalimbali, Halmashauri, Serikali kuu na wafadhili
|
4
|
Wavuvi kutumia zana duni kuvulia hivyo uvuvi kutoleta tija kwa wavuvi na uchumi
|
Kuwawezesha wavuvi kupata zana bora (boti na Injini). Wavuvi wanaweza kukopeshwa au Halmashauri kununua boti na injini na kuwakodisha wavuvi na kuwa chanzo cha mapato kwa Halmashauri na kuchangia pato la Taifa
|
5
|
Kutokuwepo kwa bwawa la kuzalishia vifaranga bora vya samaki (hatchery pond)
|
Kupatikana kwa bwawa la kuzalishia samaki kwani ufugaji wa samaki unakuwa kwa kasi lakini wafugaji wanshindwa kuzalisha kwa tija kutokana na kukosa vifaranga bora
|
6
|
Kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko
|
Kuboresha afya ya wanyama kwa kuchanja wanyama dhidi ya magonjwa ya mlipuko (kimeta, kideri, ugonjwa wa ngozi, chambavu, kichaa cha mbwa)
|
7
|
Upungufu wa watumishi
|
Idara kupatiwa watumishi kuendana na ikama. Idara ina upungufu wa watumishi 73
|
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa