Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase ameendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi wa Kata ya Lusungo Kijiji cha Kikuba tarehe 13.8.2025.
Akitatua changamoto inayotokana na kukosekana kwa mawasiliano ya barabara kipindi cha mafuriko Mhe.Manase amemtaka Mtendaji wa Kata ya Lusungokufufua na kuendeleza kamati za maafa na kuzitambulisha kwa Wananchi ili ziweze kutoa huduma za haraka ikiwemo kutambua kaya ambazo zimepatwa na maafa endapo yakitokea.
Mhe.Manase amewapongeza wananchi wa Kikuba kwa kuunga mkono suala la uchangiaji wa chakula shuleni na amewataka Wazazi waliyokwenye kamati ya chakula kulinda na kusimamia taratibu zote za utoaji wa chakula.
Aidha Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi kupitia idara ya Maendeleo ya jamii kutoa Elimu kwa Wananchi wa Kijiji cha Kikuba kuhusiana na mkopo wa 10% unaotolewa bila riba kwa Wanawake Vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kujua kanuni sheria na taratibu za kupata mkopo utakaowanufaisha na kuwainulia kipato chao.
Kuelekea katika kipindi cha Uchaguzi Mhe. Manase amewataka Wananchi wa Kikuba kujiepusha navitendo vya rushwa pamoja na matendo yoyote yatakayochochea vurugu zitakazosababisha uvunjifu wa amani kwenye jamii.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa