Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi wa Kijiji cha Mabunga kata ya Ipinda tarehe 11.8.2025
Akitatua changamoto ya kushuka kwa bei ya zao la kokoa Mhe.Manase amesema kokoa inauzwa kwa njia ya mnada kupitia soko la dunia, hivyo bei inapangwa kulingana na uzalishaji na uhitaji, pia amewaasa viongozi wa vyama vya ushirika (AMCOS ) kutojihusisha na masuala ya wizi wa zao la kokoa kwa yeyote atakae bainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Kuhusiana na changamoto ya uharibifu wa Miundombinu Mhe.Manase ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kununua mitambo ya kutengeneza barabara itakayosaidia kutatua baadhi ya changamoto za barabara hasa wakati wa mvua.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka Wazazi kuunga mkono sera ya Elimu bure inayotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoingozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mchango wa chakula shuleni ili kuwatengenezea watoto Afya ya mwili na akili pamoja na kujenga ushirikiano mzuri baina yao.
akisisitiza matumizi ya nishati safi Mhe. Manase amesema mpango wa Serikali ni kupeleka umeme kwenye vijiji na vitongoji hivyo mpango huo utasaidia Wananchi kuacha matumizi ya nishati chafu na kutumia nishati mbadala.
Kuelekea katika kipindi cha uchaguzi Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Kyela amewataka wananchi kujiepusha na masuala mbalimbali yatakayochochea vurugu kwenye jamii,na kuwataka kudumisha na kuendeleza amani iliyopo Nchini
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa