Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Adv.Florah A. Luhala ameongoza kikao cha tathimini ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024-2025.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 30.9.2025 ikiwa ni kwa lengo la kuboresha na kuongeza nguvu katika zoezi zima la ukusanyaji wa mapato ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyela.
Adv. Luhala amewataka Watendaji kata kusimamia vyanzo vya mapato vilivyopo kwenye kata zao na kuwataka kuwasimamia vizuri mawakala ili waweze kutuma fedha kwa wakati na kusomeka kwenye mfumo wa mapato (TAUSI) kwani fedha hizo zinatumika kwenye miradi ya maendeleo.
kuelekea katika mapokezi ya Mwenge wa uhuru unaotarajiwa kukimbizwa tarehe 11.10. 2025 Mkurugenzi amewataka viongozi ngazi ya Kata na Vijiji kuhamasisha Wananchi kwenye maeneo yao wajitokeze kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa