Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Mhe. Josphine Manase, amefunga rasmi Maonesho ya Biashara ya Kusini International Trade Fair and Festival yaliyofanyika Matema kuanzia siku za hivi karibuni na kukamilika leo tarehe 21 Septemba 2025.
Akizungumza katika hafla ya kufunga maonesho hayo, Mhe. Manase aliwapongeza wafanyabiashara mbalimbali walioshiriki kwa kuonesha bidhaa na huduma zao, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sekta mbalimbali muhimu ikiwemo kilimo, uvuvi na biashara.
Aidha, alibainisha kuwa lengo kuu la maonesho hayo ni kuwaunganisha wananchi na wafanyabiashara katika kuzitambua na kuzifanyia kazi fursa zilizopo ndani ya Wilaya ya Kyela, ili hatimaye ziwe chachu ya kuinua uchumi wa wananchi na wilaya kwa ujumla.
DC Manase pia amewasisitiza wafanyabiashara kutumia mitandao ya kijamii kama nyenzo muhimu ya kutangaza bidhaa na fursa zao, akisema teknolojia ya kidigitali imekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya biashara duniani.
Vilevile, Mhe. Manase aliwahimiza wajasiriamali wa ndani ya Kyela kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kila mara matamasha kama haya yanapofanyika, ili wapate nafasi ya kuonesha bidhaa zao na kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazopatikana ndani ya wilaya ya Kyela.
Mwisho DC Manase amewaasa waandaaji wa Kusini International Trade Fair and Festival kuendeleza ushirikiano na wadau waliokutana nao mwaka huu, ili kutumia uzoefu na mapendekezo yao katika kuandaa tamasha jingine kubwa na bora zaidi mwakani.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa