Haya yamezungumzwa na naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Tixon Tuliangine Nzunda, alipokuwa akiongea na Wakuu wa shule, Walimu wakuu, pamoja na waratibu elimu katika ukumbi wa shule ya sekondari Kyela Day, iliyopo wilayani Kyela tarehe 25/01/2019.
Aidha amewataka walimu kufanya kazi kwa juhudi na maarifa makubwa, ili kuleta mabadiliko yenye tija katika elimu yetu Tanzania.
Pamoja na hayo Mhe. Tixon Mzunda alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Ndugu Lucy L. Mganga kwakutoa mchango mkubwa unaowezesha ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa wilayani hapa.
Pongezi zilitolewa kwa wilaya ya Kyela pia, kwani imejitahidi katika kufaulisha wanafunzi wengi, amesema wilayani ya Kyela imepata daraja la asilimia 52 kitaifa, na kumekuwa na ongezeko la wanafunzi 3096 wanaokwenda kuanza kidato cha kwanza, ambapo idadi hii ni kubwa ukilinganisha na miaka mingine iliyopita.
Kutokana na idadi hii ya wanafunzi kuongezeka, amewataka wakuu wa idara kwenda kuweka kambi katika maeneo yote ambapo madarasa yanajengwa, ili kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika kwa wakati, na wanfunzi wote wanajinga na kidato cha kwanza kwa masomo.
Aidha Mhe.Toxin Nzunda, amewaambia wakuu wa shule kwamba, kwa sasa wameongezewa nguvu yakuweza kuwapandisha vyeo walimu wanaofanya kazi vizuri na kuleta matokeo yenye tija. Ikiwa ni sehemu ya kuwatia moyo walimu hao.
Hata hivyo ametaja maeneo mbalimbali ambayo yatatumika katika kumpima mwalimu, ikiwemo uandaaji mzuri wa mfumo wa ujifunzaji na ufundidhaji darasani, idadi ya vipindi vilivyofundishwa kwa somo na kwa mwaka pamoja na kuangalia kiwango cha ufauru wa wanafunzi kwa somo husika.
Pia amewataka walimu wa shule za msingi kuhakikisha wanafundisha vizuri KKK, ili kuepusha kuwapeleka wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kidato cha kwanza.
Amesema, kwa asilimia 12 ya walimu wetu ni watoro kazini, asilimia 38 ya walimu hufika kazini na kusaini lakini hawaingii kufundisha. Hivyo amewataka Wakuu wa shule kusimamia nidhamu na uwajibikaji wa walimu. Endapo watashindwa wataondolewa katika madaraka na kupewa mwalimu mwingine kutoka shule hiyo.
Kuimarisha uongozi bora na ubunifu, iwe ni siraha ya kuleta mabadiliko chanya, katika kuinua taaluma mashuleni.
Inetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Ofisi ya Habari na Mahusiano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa