Kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania Mkuu wa wilaya ya Kyela, Mhe. Josephine Manase ameungana na wananchi katika zoezi la upandaji wa miti, katika kituo cha Afya cha Njisi, Kata ya Njisi, leo tarehe 23.04.2024. Ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Muungano wa Tanzania.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Manase amewataka wananchi wa Kyela, kuenzi na kudumisha Muungano huo kwa amani ili tuendelee kuishi kwa upendo.
Lakini pia Mhe. Manase Amewasisitiza wananchi, kuwaombea viongozi wetu ambao ni Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dkt. Samia Suluhu na Mwenyekiti wa Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rais. Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi kwani wanafanya kazi kubwa za kuleta maendeleo kwa wananchi.
Vilevile Mhe. Manase ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuiongoza vyema nchi yetu, katika hali ya amani na utulivu, Mhe. Manase ameendelea kwa kusema kuwa kuna baadhi ya nchi zimeshindwa kudumisha amani na Muungano hivyo kuifanyia Tanzania kuwa mfano wa kuigwa Duniani.
Mwisho Mhe. Josephine Manase amewataka wananchi kuurithisha Muungano wetu na amani kwa vizazi vyetu.
Miti 220 imepandwa leo, Wakati halmashauri ya wilaya ya Kyela inatarajia kupanda miti zaidi ya 12,000 hadi kufikia kilele cha maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanzania.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa