• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kyela District Council
Kyela District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Fedha
      • Huduma za Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Biashara na Viwanda
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • TEHAMA
  • Fursa Za uwekezaji
    • Vivutio vya Utali
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, uongozi na mipango
      • Ukimwi
      • Uchumi, ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
      • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamirika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Hatua
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu Wa Wilaya Ya Kyela Mhe. Josephine Manase Aendelea Na Ziara Yake Ya Ukaguzi Wa Miradi

Imewekwa Kwenye: April 18th, 2024

Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, tarehe 16.04.2024       ameendelea na ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika wilaya ya Kyela.

Mhe. Manase ametembelea miradi, ikiwemo ujenzi wa matundu 22 ya vyoo katika Shule ya msingi Mbogela, ujenzi wa matundu 11 ya vyoo katika shule ya msingi Kikusya, Mradi wa maji safi katika zahanati ya Kandete,ujenzi wa bwalo la wanafunzi wenye uhitaji maalumu, ujenzi wa jengo la mama na Mtoto katika kituo cha Afya cha Kilasilo,Ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Lubele na Mradi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya mkoa inayojengwa kata ya Busale.

Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Kyela amewataka Viongozi ngazi ya kata kutambua Lengo la kuletwa kwa fedha za  miradi ya Maendeleo kuwa ni kutatua kero mbalimbali za wanachi.

Aidha amewataka viongozi wa kata, kuwa makini katika usimamizi wa miradi hiyo na kuimaliza kwa wakati uliopangwa ili miradi iweze kutoa huduma katika jamii.

Pamoja na hayo, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, amewataka Viongozi na wasimamizi wa miradi Kuitambulisha miradi hiyo kwa wananchi ili kuwaweka bayana kufahamu juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo Mhe. Manase amesema hatosita kuwachukulia hatua watu wote wanaokwamisha miradi ya Maendeleo kwani kufanya hivyo nikukwamisha juhudi za Mhe. Rais.

Pia Mhe. Manase ametoa wito kwa Viongozi ngazi ya kata pindi pesa zinaposhuka kwaajili ya utekelezaji wa miradi basi pesa hizo zianze utekelezaji huo maramoja, kwani kuchelewesha utekelezaji ndio sababu ya kukwamisha miradi isimalizike kwa wakati.

Mwisho Mhe. Manase ametoa shukrani kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushusha fedha katika Wilaya ya Kyela kupitia sekta mbalimbali, pia ametoa shukrani kwa Mbunge wa jimbo la Kyela, Mhe. Ally Jumbe Mlaghila kwakuzidi kuwapambania Wananchi wa Kyela.

Matangazo

  • ORODHA YA ASASI ZILIZOPATA KIBALI CHA UANGALIZI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MWAKA 2024/2025 June 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA USAILI September 27, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • WAUGUZI WILAYANI KYELA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA MATEMA

    May 16, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA WILAYANI KYELA

    May 15, 2025
  • KAMATI YA SIASA MKOA YAPONGEZA UTEKELEZWAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KYELA

    May 14, 2025
  • WALIMU WAKUU,WALIMU WA MANUNUZI, WAKUU WA SHULE,WATENDAJI WA KATA NA WA VIJIJI WAPIGWA MSASA MFUMO WA MANUNUZI (NEST)

    April 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

Tume ya Uchaguzi
Video Zingine

Viungo Vya Haraka

  • Mbeya Region Website

Viunganishi Linganifu

  • Public Service Management
  • President's Office Regional Administration & Local Government - PORALG
  • Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
  • KYELA DISTRICT
  • KYELA DISTRICT COUNCIL

Idadi ya wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

wasiliana nasi

    Bomani Street

    Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela

    Simu ya Mezani: 025-2540035/7

    Simu ya Mkononi: 0713655466

    Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa